<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Vifo vya watu vilivyosababishwa na mlipuko wa volkano Indonesia vyaongezeka kuwa 22

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 07, 2021

    Volkano ya Semeru ikilipuka katika Wilaya ya Lumajan, Indonesia. Picha hii ilipigwa Jumatatu ya Wiki hii, Tarehe 6. (Mpigaji picha: Kurniawan)

    Shirika la Kitaifa la Kukabiliana na Maafa ya Indonesia ilisema Jumatatu ya wiki hii, Tarehe 6 kwamba, vifo vya watu vilivyosababishwa na mlipuko wa Volkano ya Semeru ya Mkoa wa Java Mashariki, Indonesia vimeongezeka na kufikia wa 22.

    Kaimu msemaji wa shirika hilo Abdul Muhari alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari kwamba, maeneo yaliyoathiriwa na volkano hiyo yako Wilaya ya Lumajan ambako kuna volkano, na nyumba za watu zipatazo 2970, shule 38 na daraja moja vimeharibiwa kwa kiasi mbalimbali. Amesema hadi saa kumi na moja ya Tarehe 6 ya saa za huko, mlipuko wa volkano umesababisha vifo vya watu 22 na wengine 27 hawajajulikana walipo.

    Muhari alisema, sasa usafiri wa baadhi ya sehemu kwenye maeneo yanayoathiriwa na maafa umekuwa ukitatizwa bado, na mvua kubwa inaleta changamoto kwa kazi za kutafuta watu waliokufa na waliojeruhiwa na uokoaji wa waathiriwa. 

    Volcano ya Semeru ikilipuka katika Wilaya ya Lumajan, Indonesia. Picha hii ilipigwa Jumatatu ya Wiki hii, Tarehe 6. (Mpigaji picha: Kurniawan)

    Volkano ya Semeru ina urefu wa mita 3,676 kutoka usawa wa bahari. Ni volkano yenye urefu zaidi kuliko nyingine zote na ni eneo linalojulikana la kupanda milima huko Java, pia ni eneo lenye volkano hai 130 hivi zinazoweza kulipuka nchini Indonesia.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha