<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi ampongeza Mattarella kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Italia

    (CRI Online) Februari 07, 2022

    Rais Xi Jinping wa China amemtumia salamu za pongezi Rais Sergio Mattarella wa Italia kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo.

    Rais Xi amebainisha kuwa China na Italia ambazo zina uhusiano wa kihistoria, kuungana mkono na zenye maslahi mapana ya pamoja, zimeweka mfano kwa jumuiya ya kimataifa katika kuaminiana, kutafuta msingi wa pamoja huku zikiondoa tofauti, na kuwa na ushirikiano wa kunufaishana.

    Vilevile Rais Xi amesema nchi hizo mbili ambazo zimepambana dhidi ya UVIKO-19 kwa nguvu zote, zinasherehekea kwa pamoja miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia wa kibalozi kati ya China na Italia, na kuungana mkono katika kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya Mwaka 2022 na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Milan ya Mwaka 2026, huku mwaka wa Utamaduni na Utalii kati ya China na Italia ukikaribia kuanza, ambapo utaleta fursa nyingi za maendeleo katika uhusiano wa pande mbili.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha