<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Kijana wa Nigeria akimbiza ndoto huko Chongqing, China

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 15, 2022

    Ifeoma Amuche Gladys akiwa katika Mashindano ya Mashairi ya China 2022. (Picha ilitolewa na Ifeoma Amuche Gladys kwa China News Service)

    Katika kipindi cha televisheni kinachopendwa sana cha “Mashindano ya Mashairi ya China 2022”, mshiriki kutoka Afrika amejitokeza kati ya washindani wake wengi.

    Ifeoma Amuche Gladys anatoka Nigeria. Jina lake la Kichina ni Chen Yue, na ndoto yake ni kujifunza utamaduni wa jadi wa China na kuhimiza ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Gladys alianza kujifunza lugha ya Kichina kwa mara ya kwanza Mwaka 2016 alipokuwa na umri wa miaka 16. Mnamo Mwaka 2018, alijiunga na Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Sichuan kilichoko Chongqing, Kusini Magharibi mwa China ili kujifunza Lugha ya Kichina ya kale.

    “Shairi la kwanza nililojifunza ni Jing Ye Si (Nawaza Usiku Tulivu )”, alisema Gladys, akaongeza kuwa “ninapenda sana shairi hilo, hivyo hakika nampenda mshairi Li Bai aliyetunga shairi hilo.”

    Baada ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Xinan mwaka 2019, aliendelea kujifunza lugha ya Kichina, akisema mashairi ni dirisha la kujifunza utamaduni unaong’ara wa China.

    Baada ya kuzama kwenye bahari ya mashairi ya jadi ya China, Gladys alijitokeza katika Kipindi cha televisheni cha “Mashindano ya Mashairi ya China 2022”.

    Kijana huyu alisema, ana tumaini la kuwa mkalimani wa mikutano baada ya kuhitimu masomo chuoni. 

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha