<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Marais wa China na Indonesia wafanya mazungumzo kwa njia ya simu

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2022

    BEIJING - Rais wa China Xi Jinping Jumatano wiki hii amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Indonesia, Joko Widodo.

    Katika mazungumzo hayo, Xi amesema China na Indonesia zote ni wawakilishi wa nchi kubwa zinazoendelea na nchi zinazoinukia kiuchumi.

    Katika kukabiliwa na mabadiliko makubwa ya kimataifa na janga la UVIKO-19, yote mara chache kutokea katika karne, Xi amesema, nchi hizo mbili zimesonga mbele pamoja na kukabiliana na changamoto, zimeanzisha njia mpya za ushirikiano wa pande mbili wenye kuimarika vema wa masuala ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na baharini, na kuendeleza ajenda kuu ya mshikamano dhidi ya janga na maendeleo ya pamoja.

    Xi ameongeza kwamba, nchi hizo mbili zimeweka mwelekeo wa jumla wa kujenga kwa pamoja jumuiya ya China na Indonesia yenye mustakabali wa pamoja, na kuweka mfano wa ushirikiano wa dhati kati ya nchi kubwa zinazoendelea..

    Xi amesisitiza kuwa pande hizo mbili zinapaswa kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kuhusu masuala kama vile kuimarisha ushirikiano wa chanjo dhidi ya UVIKO-19, na kuendelea kuimarisha ushirikiano katika kupambana na janga hilo.

    Amesema kwamba, pande zote mbili zinapaswa kuhakikisha kuwa Reli ya Treni za Mwendo Kasi ya Jakarta-Bandung inaanza kufanya kazi katika muda uliopangwa, kutekeleza vema miradi muhimu ikiwemo ukanda wa uchumi wa kina wa kikanda na "Nchi Mbili, Bustani Pacha," na kwa pamoja kujenga Ukanda na Njia kwa ubora wa juu, ili kusaidia kuharakisha maendeleo ya Indonesia na ushirikiano wa nchi mbili.

    Xi ametoa wito kwa pande zote mbili kudumisha soko thabiti la kimataifa na minyororo ya ugavi bidhaa duniani kote, kukuza utekelezaji thabiti wa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, kulinda kithabiti usanifu wa kikanda unaozingatia ASEAN ambao uko wazi na jumuishi, na kuendelea kujitolea kudumisha umoja na ushirikiano kwa faida za pande zote na kunufaishana.

    Ameongeza kwamba, China inaunga mkono Indonesia katika kutekeleza jukumu lake la kuwa mwenyekiti wa mzunguko wa Kundi la nchi 20 tajiri duniani (G20), na kuzingatia kaulimbiu ya "Fufuka Pamoja, Fufuka Imara," ili kuhakikisha Mkutano wa G20 wa Bali wa Mwaka 2022 unafanikiwa.

    Kwa upande wake, Widodo ameipongeza China kwa kuhitimisha kwa mafanikio "mikutano mikuu miwili" ya kila mwaka pamoja na Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Majira ya baridi ya Beijing.

    Pia ametaja miradi ya Reli ya Kasi ya Jakarta-Bandung, ujenzi wa mji mkuu mpya wa Indonesia, na Pendekezo la Maendeleo ya Kimataifa lililopendekezwa na Xi kuwa miradi muhimu ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili na kwamba China inaweza kusaidia Indonesia kukamilisha na kushiriki miradi hiyo.

    Widodo amesisitiza kwamba Indonesia iko tayari kudumisha mawasiliano ya karibu na China ili kusukuma mbele utekelezaji wa mipango na miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa maeneo maalumu ya viwanda wa ajili ya maendeleo ya pamoja ya Dunia.

    Pande hizo mbili pia zimebadilishana mawazo kuhusu hali ya Ukraine na kukubaliana kwamba pande zote zinapaswa kushikamana na kuendeleza mazungumzo ya amani, kuzuia mzozo mkubwa wa kibinadamu, kudhibiti athari mbaya za vikwazo kwa uchumi wa Dunia na kuepuka kuzorotesha mchakato wa kufufua uchumi wa Dunia.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha