<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais wa China asisitiza jukumu la nchi jirani katika kuunga mkono Afghanistan

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 31, 2022

    BEIJING - Rais wa China Xi Jinping leo Alhamisi ametoa wito kwa nchi jirani na Afghanistan kujitahidi kusaidia watu wa Afghanistan kujenga mustakabali mzuri zaidi.

    Xi ameyasema hayo kwenye salamu zake za maandishi alizotuma kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi jirani na Afghanistan, unaofanyika mjini Tunxi, katika Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China.

    Xi ameeleza kwamba baada ya kukabiliana na changamoto nyingi siku zilizopita, Afghanistan inahitaji maendeleo ya haraka katika maeneo mengi. Nchi hiyo imefikia kipindi muhimu cha mabadiliko kutoka kwenye machafuko hadi utulivu.

    "Afghanistan ni jirani na mshirika mwenzi wa pamoja wa nchi zote zinazoshiriki, na tunajenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja inayounganishwa na milima na mito, inayoinuka na kushuka pamoja," Xi amesema.

    Vile vile amesema kuwa Afghanistan yenye amani, utulivu, maendeleo na ustawi ni matarajio ya watu wote wa Afghanistan, na pia inaendana na maslahi ya pamoja ya nchi za kanda hiyo na jumuiya ya kimataifa.

    Xi amesisitiza kwamba urafiki na ujirani mwema ni muhimu kwa nchi.

    Rais Xi amesema China daima inaheshimu mamlaka ya Afghanistan, uhuru na ukamilifu wa eneo lake, na imejitolea kuunga mkono juhudi za Afghanistan za kutafuta amani, utulivu na maendeleo.

    Amesema kwamba, utaratibu wa uratibu na ushirikiano kati ya nchi jirani na Afghanistan tangu uanzishwe Mwezi Septemba mwaka jana, umejitahidi kutumia nguvu za nchi jirani, na hivyo kuchukua jukumu la kiujenzi katika kukuza mpito thabiti nchini Afghanistan.

    Xi amesisitiza kuwa, nchi jirani na Afghanistan zinapaswa kufanya ziwezavyo ili kujenga maelewano na kuratibu juhudi za kuwaunga mkono watu wa Afghanistan katika kujenga mustakabali mwema.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha