<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Hadithi ya Simuxin Ding ya enzi ya Yin

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 21, 2022

    Magofu ya Enzi ya Yin yako kwenye kitongoji cha Kaskazini Magharibi ya Anyang, mji maarufu wa historia na utamaduni wa China, yakipita kando mbili za Mto Huan. Wakati wa zama za kale mji huo uliitwa “Bei Meng”, au “Jiji Yi Shang”, “Yi Shang”. Haya ni magofu ya kwanza ya jiji la kale nchini China ambayo yamethibitishwa na nyaraka za kihistoria pamoja na mabaki ya kale ya maandishi yaliyochongwa kwenye mifupa iliyofukuliwa, yakiwa na historia ya miaka 3300.

    Habari zinasema, kaburi la Fu Hao lilifukuliwa na watafiti wa makaki ya kale mwaka 1976. Ndani ya kaburi hilo kuna mabaki mbalimbali ya kale 1928 kwa jumla kama vile vyombo vya shaba nyeusi na sanaa za jade na mengineyo. Katika mabaki haya ya kale, Simuxin Ding, yaani chombo cha shaba nyeusi kinachoitwa Simuxin ni hazina yenye thamani zaidi kwenye Jumba la Makumbusho la Magofu ya Enzi ya Yin. Chombo hicho cha shaba nyeusi cha kale cha China ni chenye miguu minne. Kimo cha Chombo hiki ni sentimita 80.1, na mzingo wa mdomo wake wa mraba kwa jumla ni sentimita 64.

    “Mmiliki wa chombo hicho alikuwa malkia maarufu katika historia ya China Fu Hao, ambaye pia alikuwa Jenerali mwanamke hodari.” Mkurugenzi wa Jumba la Makumbusho la Enzi ya Yin Guo Weibing alijulisha kuwa, Fu Hao alikuwa na uwezo mkubwa sana, siyo tu aliweza kumsaidia mume wake Mfalme Wuding kushughulikia mambo ya utawala , bali pia alikuwa na vipaji vya kijeshi. Majeshi ya Yin yalishinda katika karibu kila vita chini ya uongozi wake, alipata mafanikio makubwa katika vita kwa ajili ya enzi hiyo ya kifalme. Mfalme Wu Ding si kama tu alitoa zawadi kubwa ya ardhi kwa malkia wake, bali pia alimruhusu aongoze shughuli kubwa za matambiko kwa mara nyingi.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha