<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Korea Kusini watumiana pongezi kuadhimisha miaka 30 ya uhusiano wa kidiplomasia

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 25, 2022

    BEIJING - Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Korea Kusini, Yoon Suk-yeol, Jumatano wiki hii walitumiana salamu za pongezi kwa kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

    Katika ujumbe wake, Xi amesema kuwa China na Korea Kusini ni majirani wa kudumu wanaopakana kwa ukaribu na ng'ambo ya bahari, na watu wa nchi hizo wanafurahia historia ndefu ya mabadilishano ya kirafiki.

    “Tangu China na Korea Kusini zianzishe uhusiano wa kidiplomasia miaka 30 iliyopita, uhusiano wa nchi hizo mbili kwa juhudi za pamoja za pande zote mbili, umekuwa ukiendana na wakati, umeendelezwa kwa njia ya pande zote na kupata matokeo yenye matunda, hali ambayo imeleta manufaa makubwa kwa nchi hizo mbili na watu wake, na pia imetoa mchango mkubwa kwa amani na maendeleo ya kikanda na Dunia,” Xi amesema.

    Xi ameeleza kuwa, ni kwa sababu nchi hizo mbili zinaheshimiana na kuaminiana, kushughulikia masilahi ya msingi ya kila mmoja na masuala makuu yanayofuatiliwa kwa pamoja, na kuongeza maelewano na uaminifu kupitia mawasiliano ya dhati.

    Xi ameweka bayana sababu nyingine ya mafanikio hayo makubwa ni kwamba nchi hizo mbili zinafuata ushirikiano na kupata matokeo yenye manufaa kwa pande zote, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana, mabadilishano na kujifunza kwa pamoja, ili kupata mafanikio na ustawi wa pamoja.

    “Pia ni kwa sababu nchi hizo mbili zimesisitiza juu ya uwazi na ujumuishaji, na zimeshirikiana pamoja kulinda amani na utulivu wa kikanda, kuhimiza maendeleo jumuishi ya kikanda, na kudumisha kanuni za msingi zinazoongoza uhusiano wa kimataifa,” Xi amesema, huku akiongeza kuwa uzoefu huo muhimu hapo juu unapaswa kuthaminiwa kwa uangalifu mkubwa na kuzingatiwa kwa muda mrefu.

    Xi amesema, kwa sasa, Dunia imeingia katika kipindi kipya cha misukosuko na mageuzi chini ya athari za pamoja za mabadiliko ya kimataifa na janga la UVIKO-19, ambazo zote hazijapata kuonekana katika karne moja iliyopita. Amesema, katika wakati huu muhimu, jumuiya ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na China na Korea Kusini, inaweza tu kuondokana na migogoro na wimbi la matatizo kupitia mshikamano na ushirikiano. Ameongeza kuwa, nchi hizo mbili zinapaswa kuwa majirani wazuri, marafiki wazuri na washirika wazuri.

    Katika salamu zake za pongezi, Yoon ametoa pongezi za dhati kwa maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Korea Kusini na China.

    Huku akiweka bayana kuwa Korea Kusini na China ziko karibu kijiografia na zinafurahia uhusiano wa kihistoria na kiutamaduni unaoheshimiwa kwa muda mrefu, amesema tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia Mwaka 1992, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta za siasa, uchumi na utamaduni umeshuhudia maendeleo makubwa ya kupiga hatua, na ushirikiano wenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili umeendelea kuimarishwa.

    Siku hiyo hiyo, Waziri Mkuu wa China Li Keqiang pia alitumiana salamu za pongezi na Waziri Mkuu wa Korea Kusini Han Duck-soo.

    Katika salamu zake, Li amesema kuwa China na Korea Kusini ni majirani wa karibu wa kudumu ambao hawawezi kuondoka, na pia ni washirika wenzi wasioweza kutenganishwa.

    Amesema, upande wa China uko tayari kushirikiana na Korea Kusini kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia ikichukulia kama hatua mpya ya kuanzia ili kuongeza maelewano na kuaminiana.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha