<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi atoa barua ya pongezi kwa Baraza la 5 la ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya China na Afrika

    (CRI Online) Agosti 26, 2022

    Rais Xi Jinping wa China leo ametoa pongezi kwa Baraza la 5 la ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya China na Afrika, lililofunguliwa tarehe 25 hapa Beijing.

    Rais Xi amesema China na nchi za Afrika zina muskabali wa pamoja, vyombo vya habari vya pande hizi mbili vinabeba majukumu makubwa katika kuimarisha hali ya kuaminiana na ushirikiano, kulinda amani ya dunia, na kuhimiza maendeleo duniani.

    Rais Xi amesema katika miaka 10 iliyopita tangu baraza hilo lianzishwe, vyombo vya habari vya China na Afrika vimetoa jukwaa muhimu la kuongeza mawasiliano na ushirikiano kati ya pande mbili, na kufanya kazi muhimu kwa ajili ya kuhimiza mawasiliano na kufundishana kati ya pande mbili katika sekta ya utamaduni, na kuimarisha uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote kati ya China na Afrika.

    Rais Xi ameeleza matumaini yake kuwa vyombo vya habari vya pande hizo mbili vitachangia kusimulia vizuri hadithi kuhusu China na Afrika katika zama mpya, kueneza maadili ya pamoja ya binadamu na kuhimiza kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha