<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Xi Jinping na Macky Sall wapongezana kwa miaka 20 ya kuanzishwa kwa AU na uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na AU

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 09, 2022

    Tarehe 9, Septemba, rais Xi Jinping wa China na rais wa Senegal Macky Sall, ambaye pia ni Mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika (AU) walitumiana barua ya pongezi kwa kuadhimisha miaka 20 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika na ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Umoja wa Afrika.

    Rais Xi alidhihirisha kuwa , katika miaka 20 iliyopita, Umoja wa Afrika ukiongoza nchi za Afrika kusonga mbele kwenye njia ya kushirikiana na kujikakamua, kujiendeleza na kustawisha na kufanya ujenzi wa utandawazi, na umeonesha nguvu ya Afrika katika kupambana na maambukizi ya virusi vya korona, kufanya ushirikiano wa pande nyingi, na kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea. China na Afrika ni marafiki wakubwa, wenzi wema na ndugu wanaoungana mkono kwa karibu tangu zamani. Ninatilia maanani maendeleo ya uhusiano kati ya China na Umoja wa Afrika, na ningependa kufanya juhudi pamoja na rais Sall na marais wa nchi wanachama wengine wa Umoja wa Afrika, kwa kuchukulia maadhimisho ya miaka 20 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Umoja wa Afrika kuwa mwanzo mpya, ili kutoa mchango mpya kwa ajili ya ujenzi wa jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.

    Rais Sall alisema, wakati wa maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika, rais Xi Jinping amenitumia barua ya pongezi yenye uchangamfu, ambayo inaonesha urafiki wa karibu wa watu wa Afrika na China, ningependa kukushukuru kwa dhati. Ninasifu sana urafiki wa jadi wa Afrika na China, mshikamano na ushirikiano , na uhusiano wa kiwenzi chini ya mfumo wa Baraza la Ushirikiano la China na Afrika kati ya pande hizo mbili. Ninasisitiza kuwa, upande wa Afrika unaunga mkono kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja duniani, na kuunga mkono kithabiti Bara la Afrika kushirikiana na China ya kirafiki katika kujenga pamoja jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya pamoja na China.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha