<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping wa China ahudhuria mkutano wa sita wa wakuu wa nchi za China, Russia na Mongolia

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 16, 2022

    Rais Xi Jinping wa China akiongoza mkutano wa sita wa wakuu wa nchi za China, Russia na Mongolia na mwenzake wa Russia, Vladimir Putin, na wa Mongolia, Ukhnaa Khurelsukh, kwenye ukumbi wa Forumlar Majmuasi huko Samarkand, Uzbekistan, Septemba 15, 2022. (Xinhua/Zhai Jianlan)

    SAMARKAND, Uzbekistan - Rais wa China Xi Jinping amehudhuria kwenye mkutano wa sita wa wakuu wa nchi za China, Russia na Mongolia Alhamisi mchana akiwa na mwenzake wa Russia, Vladimir Putin, na wa Mongolia, Ukhnaa Khurelsukh, kwenye Ukumbi wa Forumlar Majmuasi huko Samarkand.

    Katika mkutano huo, Xi amesisitiza msukumo mkubwa na uthabiti wa ushirikiano kati ya China, Russia na Mongolia.

    Licha ya athari za janga la UVIKO-19, ushirikiano wa pande tatu haujawahi kusimamishwa, na mafanikio yaliyopatikana yanapaswa kutambuliwa, amesema Xi, na kuongeza kuwa nchi hizo tatu zimepambana na janga hilo kwa pamoja, kutuma vifaa tiba kwa kila mmoja kwa wakati wa mapema iwezekanavyo, kushiriki uzoefu wa kupambana na janga hilo bila kuchoka, na kulinda kwa pamoja maisha na afya ya watu wao.

    Xi amesema, nchi hizo tatu, zimekuwa na majadiliano ya mtandaoni ili kudumisha kasi ya mabadilishano, na mioyo ya watu wa pande zote ililetwa karibu zaidi.

    Xi ametoa pendekezo lenye vipengele vinne kuhusu kuendeleza ushirikiano kati ya China na Russia na Mongolia: Kwanza, kudumisha ushirikiano wa pande tatu katika mwelekeo sahihi. Amesema, ni muhimu kuimarisha kuaminiana kisiasa, kuongeza msaada wa pande zote, kuheshimiana na kushughulikia masilahi ya kimsingi ya kila mmoja na masuala makuu, na kuimarisha uratibu na ushirikiano katika masuala ya kimataifa na kikanda.

    Pili, kuboresha ushirikiano ndani ya mfumo wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ili kujenga kwa pamoja jukwaa la ushirikiano dhidi ya hatari na changamoto na jukwaa la ukuaji kiuchumi linalosaidia kuibua uwezo wa maendeleo.

    Tatu, kufuata maelewano ya pamoja yaliyofikiwa kuhusu ujenzi wa Ukanda wa Kiuchumi wa China-Mongolia-Russia, kuunga mkono kanda jirani katika kuimarisha ushirikiano katika uchumi na biashara, mabadilishano kati ya watu, utalii na nyanja nyinginezo, na kuendelea kujenga majukwaa yenye ubora wa juu kwa mabadilishano ya jumuiya za wafanyabiashara wa nchi hizo tatu.

    Nne, kufanya kazi zenye matokeo zaidi katika ushirikiano wa pande tatu na kuunga mkono upanuzi wa matumizi ya fedha za nchi husika katika biashara ya pande zote. Xi amesema, mashirika ya kifedha ya Russia na Mongolia yanakaribishwa kujiunga na Mfumo wa Malipo wa Benki wa Kuvuka Mipaka wa Yuan ili kujenga ngome thabiti ya usalama wa kifedha katika eneo hili.

    Naye Putin amesema kuwa ushirikiano wa pande tatu kati ya Russia, China na Mongolia umepata mafanikio makubwa, na kwa hali yake ya kunufaishana, unaongeza thamani katika maendeleo ya uhusiano wao wa pande zote.

    Putin amesema, nchi hizo zikiwa ni majirani wa karibu, zinapaswa kuwa na maelewano ya pamoja na kusaidiana, na kujumuisha na kukuza ushirikiano wa pande tatu.

    Kwa upande wake Khurelsukh amesema kuwa maendeleo ya ushirikiano wa ujirani mwema na wa kirafiki kati ya China na Russia ni kipaumbele cha kidiplomasia kwa Mongolia.

    “Kwa kuzingatia hali tata ya kimataifa, ni muhimu zaidi kuimarisha ushirikiano wa pande tatu kati ya Mongolia, China na Russia,” amesema.

    Rais Xi Jinping wa China akiongoza mkutano wa sita wa wakuu wa nchi za China, Russia na Mongolia na mwenzake wa Russia, Vladimir Putin, na wa Mongolia, Ukhnaa Khurelsukh, kwenye ukumbi wa Forumlar Majmuasi huko Samarkand, Uzbekistan, Septemba 15, 2022. (Xinhua/Zhai Jianlan)

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha