<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping akutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Pakistan

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 03, 2022

    Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Pakistani Shahbaz Sharif kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Novemba 2, 2022. (Xinhua/Yao Dawei)

    BEIJING - Rais wa China Xi Jinping Jumatano wiki hii katika Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, China amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Muhammad Shehbaz Sharif wa Pakistani ambaye yuko kwenye ziara yake rasmi nchini China.

    Xi amemkaribisha Sharif na kumshukuru kwa barua yake ya pongezi mara baada ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).

    Akiweka bayana kuwa China na Pakistan ni marafiki wazuri, washirika wazuri na ndugu wazuri, Xi amesema licha ya mabadiliko na ukosefu wa utulivu duniani katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo mbili zimesaidiana na kusonga mbele, na kuonyesha urafiki wa hali ya juu.

    "China inatendea uhusiano wake na Pakistan kwa mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, na Pakistan daima imekuwa kipaumbele cha juu katika diplomasia ya ujirani mwema ya China," Xi amesema.

    Xi amesema, China iko tayari kushirikiana na Pakistan ili kuinua kiwango cha ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, kuharakisha juhudi za kujenga jumuiya ya karibu ya China na Pakistan yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya, na kutia msukumo mpya katika ushirikiano wao wa wenzi wa kimkakati wa siku zote.

    Baada ya kujulisha mafanikio yaliyopatikana kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, Xi amesisitiza kwamba China itaendeleza sera yake ya msingi ya kufungua mlango na kutoa fursa mpya kwa Pakistan na Dunia nzima kupitia maendeleo endelevu.

    Xi amesema China itazidisha mafungamano ya mikakati yake ya maendeleo na ile ya Pakistan, akitoa wito kwa pande hizo mbili kutumia kikamilifu Kamati ya Ushirikiano ya Pamoja ya Ukanda wa Kiuchumi wa China na Pakistan (CPEC), kuendeleza CPEC kwa ufanisi zaidi, na kuifanya CPEC kuwa kielelezo cha ushirikiano wa hali ya juu wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.

    Amesema China itaendelea kufanya kila iwezalo kuiunga mkono Pakistan katika kuleta utulivu wa hali yake ya kifedha. China inaunga mkono mikoa yake yenye maendeleo ya kiviwanda katika kuungana na washirika wa Pakistan ili kuendeleza ushirikiano wa kiviwanda, na inatumai kuwa upande wa Pakistan utaweka mazingira mazuri ya biashara.

    Xi ameelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu usalama wa raia wa China nchini Pakistan, na kueleza matumaini yake kwamba Pakistan itatoa mazingira ya kuaminika na salama kwa mashirika na makampuni ya China na wafanyakazi wanaofanya kazi katika miradi ya ushirikiano huko.

    Xi amesema China itashirikiana na Pakistan kuendeleza utekelezaji wa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia na Pendekezo la Usalama wa Dunia, ili kufanya mfumo wa usimamizi wa kiuchumi duniani kuwa wenye haki, usawa zaidi, unaojumuisha watu wote na wenye manufaa kwa pande zote, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    “Jitihada hizi za ushirikiano zitatoa msingi imara kwa maendeleo ya nchi hizi mbili, na kuchangia zaidi katika amani, utulivu na ustawi wa Dunia,” Xi amesema.

    Kwa upande wake Sharif, ameeleza kuwa ni heshima kubwa kwake kuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza wa kigeni kuzuru China baada ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC wenye mafanikio, ambao umeashiria hatua mpya. Amesema ziara hiyo ni ushahidi wa urafiki wa dhati kati ya Pakistan na China.

    Kwa niaba ya serikali na wananchi wa Pakistan, Sharif kwa mara nyingine tena ametoa pongezi za dhati kwa Rais Xi kwa kuchaguliwa tena kuwa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC. Amesema katika muongo mmoja uliopita, chini ya uongozi mahiri wa Rais Xi, China imefanya muujiza ya mafanikio makubwa ya kimaendeleo.

    Sharif amesisitiza kwamba kuimarisha ushirikiano wa kimkakati wa siku zote kati ya Pakistani na China ni msingi wa sera ya nje ya Pakistan na makubaliano ya kitaifa ya Pakistan. 

    Rais wa China Xi Jinping akikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Pakistani Shahbaz Sharif katika Jumba Kuu la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Novemba 2, 2022. (Xinhua/Xie Huanchi)

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha