<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Xi apongeza Shirika la Kimataifa la Mianzi na Mihinzilani kwa kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 08, 2022

    BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma barua ya pongezi siku ya Jumatatu kwa Maadhimisho ya Miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Kimataifa la Mianzi na Mihinzilani (INBAR) na Kongamano la Pili la Dunia la Mianzi na Mihinzilani.

    Xi amesema, tangu kuanzishwa kwake, shirika hilo limejitolea kulinda, kuendeleza na kutumia rasilimali za mianzi na mihinzilani, na limekuwa na jukumu la kiujenzi katika kuhimiza ulinzi wa kiikolojia na mazingira duniani pamoja na maendeleo endelevu.

    “Serikali ya China na shirika hilo wameungana kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Dunia na kwa pamoja wamezindua mpango wa mianzi kama mbadala wa mpango wa plastiki ili kuhimiza nchi kupunguza uchafuzi unaotokana na plastiki, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030 ya Maendeleo Endelevu” amesema.

    Xi amesisitiza kuwa China imekuwa ikihimiza kwa nguvu maendeleo ya kiikolojia na kufuata dhana ya maendeleo ya kuishi pamoja kwa mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili.

    China inapenda kuendelea kushirikiana na pande zote kujenga jumuiya ya maisha ya binadamu na mazingira ya asili na kujenga Dunia safi na nzuri kwa ajili ya vizazi vijavyo.

    Shughuli za Maadhimisho ya Miaka 25 ya INBAR na Kongamano la Pili la Mianzi na Mihinzilani Duniani, kwa pamoja zikiwa na kaulimbiu ya "Mianzi na Mihinzilani - Suluhu za Mazingira Asilia kwa Maendeleo Endelevu," zimefunguliwa Beijing siku ya Jumatatu.

    Hafla hiyo ya maadhimisho imeandaliwa kwa pamoja na Idara ya Taifa ya Misitu na Uoto Asilia ya China na INBAR.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha