<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping akutana na Waziri Mkuu wa Italia Meloni

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 17, 2022

    Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni kisiwani Bali, Indonesia, Novemba 16, 2022. (Xinhua/Shen Hong)

    BALI, Indonesia - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni Jumatano jioni.

    Kwenye mkutano huo, Xi amesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, China na Italia zimeshirikiana bega kwa bega kukabiliana na UVIKO-19, na kufanya shughuli za Mwaka wa Utamaduni na Utalii wa China na Italia katika kila nchi hizo mbili na vilevile Maonyesho ya ustaarabu"Tota Rome ya Kale: Asili ya Italia ” nchini China, ikionyesha wazi urafiki na mabadilishano kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Xi amesema, China na Italia zikiwa ni nchi zenye ustaarabu wenye historia ndefu, ni wenzi wa kimkakati wa pande zote ambao wana maslahi mapana na msingi wa ushirikiano.

    “Ni muhimu kwa nchi hizi mbili kuendeleza mila na desturi za urafiki, kuelewa na kuunga mkono maslahi ya msingi na ufuatiliaji wa kila mmoja na mambo yanayohusu maslahi makuu, kutafuta maoni ya pamoja huku zikiweka kando tofauti, kupanua maelewano, na kuweka mfano wa uhusiano kati ya nchi zenye mifumo tofauti ya kijamii na asili tofauti ya kitamaduni,” Xi amesema.

    Xi amesisitiza matumaini yake kuwa nchi hizo mbili zitatumia Kamati ya Serikali ya China na Italia na mfumo wa mazungumzo katika sekta mbalimbali ili kutafuta uwezekano wa ushirikiano katika maeneo kama vile viwanda vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu, nishati safi, usafiri wa ndege na anga ya juu na katika masoko ya nchi nyingine.

    China itaendelea kujitolea katika kufungua mlango kwa kiwango cha juu na itaagiza bidhaa zenye ubora zaidi kutoka Italia, Xi amesema, huku akiongeza kuwa China inaikaribisha Italia kuwa mgeni rasmi wa Maonesho ya Kimataifa ya Wanunuzi Bidhaa ya China ya Mwaka 2023.

    Rais Xi amesema, pande hizo mbili zinahitaji kuinua Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Mwaka 2026 huko Milan ili kuongeza ushirikiano katika michezo ya majira ya baridi na viwanda.

    Xi pia ameelezea umuhimu wa kuhimiza ukuaji thabiti wa uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya.

    Kwa upande wake, Meloni ameelezea furaha yake kupata fursa ya kukutana na Rais Xi.

    Italia na China zote zina ustaarabu wenye historia ndefu, na zina jadi ya muda mrefu ya urafiki na mabadilishano, amesema, huku akiongeza kuwa upande wa Italia unafurahi kuona shughuli za Mwaka wa Utamaduni na Utalii zinafanyika, na iko tayari kuendelea kuhimiza ushirikiano wa nchi mbili katika sekta za biashara na utamaduni.

    Meloni amesema Italia haikubaliani na makabiliano ya kambi na inaamini kwamba nchi zinapaswa kuheshimu tofauti na migongano, kuimarisha mshikamano, kudumisha mazungumzo na mabadilishano, na kuongeza maelewano.

    Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni kisiwani Bali, Indonesia, Novemba 16, 2022. (Xinhua/Shen Hong)

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha