<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping asisitiza maendeleo yenye ubora wa juu katika juhudi za maendeleo ya kisasa ya China

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 06, 2023

    Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akishiriki kwenye majadiliano ya wajumbe wa ujumbe wa Mkoa wa Jiangsu kwenye Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) hapa Beijing, Machi 5, 2023. (Xinhua/Li Xueren)

    BEIJING - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) Jumapili amesisitiza kwamba maendeleo yenye ubora wa juu ni kazi ya kwanza na kipaumbele cha juu zaidi katika kujenga nchi ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa katika mambo yote.

    Rais Xi, amesisitiza hayo akishiriki kwenye majadiliano ya wajumbe wa ujumbe wa Mkoa wa Jiangsu kwenye Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) hapa Beijing, China.

    Rais Xi amesema, “Jitihada zinapaswa kufanywa ili kutekeleza wazo jipya la maendeleo kwa ukamilifu, usahihi na kwa pande zote , na kushikilia uongozi wa pamoja wa kazi zote za uvumbuzi, uratibu, uhifadhi ya mazingira, kufungua mlango na kunufaika pamoja,ili kusukuma mbele maendeleo, kuratibu vizuri zaidi kazi zenye ufanisi wa kuinua maendeleo na kupata ongezeko la kufaa, kushikilia maendeleo yenye ubora wa juu, na kutoa kipaumbele ufanisi na manufaa yake. Amesema, ni lazima nchi ya China iendeleze kwa kina mageuzi na kufungua mlango bila kuyumbayumba, na kubadilisha kwa kina njia yake ya kujipatia maendeleo, ili kuanzisha haraka mifumo na taratibu za maendeleo endelevu ya kiwango cha juu. Rais Xi amesema, maendeleo ya China lazima yaendelee kutoka mwanzo na msingi wa kukidhi mahitaji ya watu yanayoongezeka siku hadi siku juu ya maisha bora, na kuyawezesha mafanikio ya maendeleo yawe ubora wa maisha siku hadi siku ili watu wawe na hisia za kujipatia furaha na usalama.

    Rais Xi amesema kuharakisha juhudi za kujiimarisha na kuwa na nguvu katika sayansi na teknolojia ni njia ambayo China inapaswa kuchukua ili kuendeleza maendeleo yenye ubora wa juu.

    “Ili kufungua maeneo mapya na nyanja mpya za maendeleo na kuhimiza vichochezi vipya vya ukuaji wa uchumi na nguvu mpya katika kukabiliana na ushindani mkali wa kimataifa, China inapaswa hatimaye kutegemea uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia” amesema Rais Xi

    Amewaambia wajumbe hao wa Bunge la Umma la 14 la China kwamba juhudi lazima zifanywe kujenga vituo vya uvumbuzi vya sayansi na teknolojia vyenye ushawishi duniani na kuimarisha mageuzi ya mfumo wa kisayansi na kiteknolojia.

    Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akishiriki kwenye majadiliano ya wajumbe wa ujumbe wa Mkoa wa Jiangsu kwenye Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) hapa Beijing, Machi 5, 2023. (Xinhua/Huang Jingwen)

    Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akishiriki kwenye majadiliano ya ujumbe wa Mkoa wa Jiangsu kwenye Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) hapa Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 5, 2023. (Xinhua/Huang Jingwen)

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha