<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais wa China ampa salamu za pole mwenzake wa DRC kufuatia nchi hiyo kukumbwa na maafa ya mvua kubwa

    (CRI Online) Mei 12, 2023

    Rais Xi Jinping wa China siku ya Alhamisi alimpa salamu za pole mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi kufuatia nchi hiyo kukumbwa na maafa ya mvua kubwa, ambayo imesababisha vifo na majeruhi kwa watu wengi na hasara kubwa za kiuchumi nchini humo.

    Rais Xi, kwa niaba ya Serikali na watu wa China, ametoa salamu za rambirambi kwa wafiwa na pole kwa majeruhi na waathirika wa maafa hayo. Amesema anaamini kuwa watu wa DRC hakika wataweza kushinda changamoto na kujenga upya maskani yao.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha