<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi asisitiza maendeleo ya utamaduni katika barua yake kwa Baraza la kwanza la Kujenga Nchi yenye Nguvu ya Utamaduni

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 08, 2023

    SHENZHEN - Rais wa China Xi Jinping ametuma barua ya pongezi kwa Baraza la kwanza la Kujenga Nchi Yenye Nguvu ya Utamaduni, lililofunguliwa Jumatano huko Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China.

    Katika barua yake hiyo, Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa wito wa kuimarishwa kwa juhudi za kubeba wajibu mpya wa utamaduni, na kutoa nguvu kubwa ya kitamaduni na kiakili ili kujenga nchi yenye nguvu na kufikia ustawishaji wa Taifa la China.

    Chama cha Kikomunisti cha China kinajitahidi kupata mafanikio mapya katika kuendeleza utamaduni wa kijamaa, Rais Xi amesema katika barua hiyo, na kuongeza kuwa hatua madhubuti zimechukuliwa katika kuigeuza China kuwa nchi yenye nguvu kubwa ya utamaduni wa kijamaa tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC Mwaka 2012.

    Ametoa wito wa kufanyika kwa juhudi zaidi katika kubeba wajibu mpya wa kitamaduni, kuongeza kujiamini kitamaduni, kubaki wazi na jumuishi, kushikilia kanuni za kimsingi na kuunda msingi mpya, na kuhimiza uvumbuzi na ubunifu wa kitamaduni wa taifa zima.

    Amesema ni muhimu kuendelea kuongeza ustawi wa kitamaduni, kuifanya China kuwa nchi inayoongoza katika utamaduni, kujenga ustaarabu wa China wa zama za hivi sasa na kuhimiza mawasiliano na kufundishana kati ya ustaarabu mbalimbali.

    Li Shulei, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC, alisoma barua hiyo ya Rais Xi na kutoa hotuba muhimu katika baraza hilo.

    Baraza hilo limeandaliwa na Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC.?

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha