<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Xi Jinping atoa wito kwa Umoja wa Vijana wa Kikomunisti kubeba wajibu

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 27, 2023

    Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akikutana na wajumbe  waliochaguliwa hivi majuzi wa Kamati Kuu ya Umoja wa Vijana wa Kikomunisti wa China (CYLC) na kutoa hotuba muhimu mjini Beijing, China, Juni 26, 2023. (Xinhua/Ju Peng)

    BEIJING - Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa wito kwa uongozi mpya wa Umoja wa Vijana wa Kikomunisti wa China (CYLC) siku ya Jumatatu alipokutana na wajumbe wapya wa Kamati Kuu ya umoja huo, akiwataka kubeba kwa dhati wajibu na majukumu yao waliyokabidhiwa na CPC katika zama mpya.

    Xi amehimiza CYLC kutoa ushiriki ulio kamilifu kwa vijana wa China ili waweze kujitolea kikamilifu katika kuendeleza maendeleo ya kisasa ya China.

    Huku akieleza kuwa mustakabali wa chama na taifa ni wa kizazi kipya, Xi ameelezea matumaini yake kwamba Kamati Kuu ya Umoja wa Vijana itawahamasisha vyema vijana kushikamana na Chama ili kuendelea kuweka juhudi za kujenga nchi ya China yenye nguvu zaidi na kufikia ustawishaji wa Taifa la China.

    “Kwa lengo na dhamira iliyo wazi zaidi, maofisa wa Umoja wa Vijana wamekuwa na sura mpya miongoni mwa vijana tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC Mwaka 2012,” Xi amesema.

    Ameeleza kuwa, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, chini ya lengo la kujenga muundo mpya wa maendeleo, Umoja wa Vijana umewahamasisha wanachama wake na vijana wengine kushiriki kikamilifu katika kazi kubwa kama vile kuhimiza maendeleo yenye ubora wa juu, kupata ushindi katika mapambano dhidi ya umaskini, na kukabiliana na janga la UVIKO-19, ukionyesha ujasiri mkubwa na kujitolea kwa vijana wa China katika zama mpya.

    “Kamati Kuu ya CPC inatarajia maofisi viongozi wa Kamati Kuu ya Umoja wa Vijana watabeba jukumu la kupigiwa mfano katika kusukuma mbele kazi ya umoja huo na kazi inayohusiana na vijana,” amesema.

    Amesisitiza kuwa, kwa kuwa ni msaidizi na nguvu ya akiba ya Chama, Umoja wa Vijana lazima uelekeze kazi yake kwenye jukumu kuu la Chama katika safari mpya ya zama mpya, lililowekwa kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC.

    Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akikutana na wajumbe  waliochaguliwa hivi majuzi wa Kamati Kuu i ya Umoja wa Vijana wa Kikomunisti wa China (CYLC) na kutoa hotuba muhimu mjini Beijing, China, Juni 26, 2023. (Xinhua/Ju Peng)

    Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akikutana na wajumbe waliochaguliwa hivi majuzi wa Kamati Kuu ya Umoja wa Vijana wa Kikomunisti wa China (CYLC) na kutoa hotuba muhimu mjini Beijing, China, Juni 26, 2023. (Xinhua/Ju Peng)

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha