<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping atoa amri ya kuwapandisha cheo maafisa wa kijeshi hadi cheo cha Jenerali

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 29, 2023

    Xi Jinping, Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa kijeshi ambao wamepandishwa vyeo vyao na kuwa majenerali hapa Beijing, China, Juni 28, 2023. Rais Xi amewapa  vyeti vya amri ya kuwapandisha cheo maafisa wawili wa kijeshi hadi cheo cha Jenerali kwenye hafla iliyofanyika Jumatano. Hafla hiyo imeandaliwa na CMC mjini Beijing. (Xinhua/Li Genge)

    BEIJING - Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China ametoa vyeti vya amri ya kuwapandisha vyeo maofisa wawili wa kijeshi hadi cheo cha Jenerali kwenye hafla iliyofanyika Jumatano. Hafla hiyo imeandaliwa na Kamati Kuu ya Kijeshi mjini Beijing.

    Cheo cha Jenerali ndiyo cha daraja la juu zaidi kwa maofisa wa kijeshi ambao bado wako kazini nchini China.

    Maofisa waliopandishwa vyeo ni Zheng Xuan, kamishna wa kisiasa wa Kamandi ya Kijeshi ya Kaskazini ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China, na Ling Huanxin, kamishna wa kisiasa wa Taasisi Kuu ya Sayansi ya Kijeshi ya China.

    Kwenye hafla hiyo, Rais Xi ametoa pongezi kwa maofisa hao. Baadaye, Rais Xi na viongozi wengine walipiga picha pamoja nao.

    Zhang Youxia, naibu mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi, alitangaza amri hiyo ya kupandisha cheo, ambayo ilitiwa saini na Rais Xi.

    He Weidong, naibu mwenyekiti mwingine wakamati kuu ya kijeshi, aliongoza hafla hiyo.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha