<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping atuma barua ya pongezi kwa Mazungumzo ya tatu ya kufunzana?kati ya ustaarabu?mbalimbali

    (CRI Online) Julai 04, 2023

    Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa Mazungumzo ya Tatu ya Mabadilishano na Kufunzana kati ya Ustaarabu mbalimbali na Mkutano wa Kwanza wa Wataalamu wa Mambo ya China Duniani uliofunguliwa siku Julai 3 siku ya Jumatatu hapa Beijing.

    Kwenye barua yake, Rais Xi amebainisha kuwa katika historia ndefu ya binadamu, mataifa mbalimbali duniani yameanzisha ustaarabu wenye umaalumu na alama zao na kubadilishana kwa usawa na kufunzana kati ya ustaarabu tofauti, kutatoa mwongozo imara wa kiroho kwa binadamu kutatua changamoto za zama zao na kutimiza maendeleo ya pamoja.

    Rais Xi amesisitiza kuwa China iko tayari kushirikiana na pande mbalimbali katika kuenzi na kurithisha maadili ya pamoja ya binadamu wote ambayo ni amani, maendeleo, haki, demokrasia na uhuru, kutekeleza Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia na kusukuma mbele kwa pamoja maendeleo ya ustaarabu mbalimbali wa binadamu.

    Rais Xi pia ameeleza matumaini yake kuwa wataalamu wa mambo ya China kutoka nchi mbalimbali watakuwa mabalozi wa kuunganisha ustaarabu mbalimbali wa China na ule wa nchi za nje, na kufanya juhudi zaidi kwa ajili ya kuzidisha maelewano, urafiki na ushirikiano kati ya China na nchi za nje.

    (Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

    Picha