<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping akutana na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Henry Kissinger

    (CRI Online) Julai 20, 2023
    Rais Xi Jinping akutana na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Henry Kissinger
    (Picha inatoka CRI.)

    Rais Xi Jinping wa China leo Alhamisi hapa Beijing amekutana na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Henry Kissinger ambaye yuko ziarani nchini China.

    Rais Xi amebainisha kuwa Dkt. Kissinger ambaye ametimiza umri wa miaka 100, amefanya ziara zaidi ya 100 nchini China na kwamba 100 hizo mbili zikiwekwa pamoja, zimeipa ziara hii umuhimu maalum.

    Amesema, katika miaka 52 iliyopita, mwenyekiti hayati Mao Zedong, aliyekuwa Rais wa Marekani Richard Nixon na Dkt. Kissinger mwenyewe, walifanya uamuzi sahihi wa kuanzisha mchakato wa kurejesha kawaida uhusiano wa nchi hizo mbili, uamuzi ambao si tu umenufaisha nchi hizo mbili, bali pia umenufaisha dunia nzima.

    Rais Xi amesema, kamwe wachina hawawezi kumsahau rafiki wao mkubwa, na kamwe hawatasahau mchango wa Dkt. Kissinger katika kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano na urafiki kati ya China na Marekani.

    Kwa upande wake Dkt. Kissinger amesema ni fahari kwake kuweza kuitembelea China, na pia anaishukuru China kwa kupanga mkutano huo kwenye jengo la No. 5 katika Jumba la Wageni wa Taifa la Diaoyutai, ambako alikutana kwa mara ya kwanza na viongozi wa China.

    Dkt. Kissinger amesisitiza kuwa, uhusiano kati ya Marekani na China unahusiana na amani ya dunia na maendeleo ya jamii ya binadamu.

    (Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

    Picha