<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Xi afanya ziara ya ukaguzi kwenye kituo cha uongozi cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) katika eneo la magharibi,China

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 31, 2023

    Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa kamati kuu ya Kijeshi ya Chama (CMC), akitoa hotuba muhimu wakati wa ziara ya ukaguzi kwenye kikosi cha jeshi la anga, katika kituo cha uongozi cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) cha eneo la magharibi mwa China. Julai 26, 2023. (Xinhua/Li Gang)

    CHENGDU, Julai 30 (Xinhua)

    Rais Xi Jinping wa China amesisitiza haja ya juhudi za kuharakisha kulifanya jeshi la Ukombozi wa umma la China (PLA) kuwa la kisasa.

    Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa kamati kuu ya Kijeshi ya Chama (CMC), alisema hayo jumatano iliyopita mjini Chengdu, Mkoani Sichuan magharibi mwa China, wakati wa ziara ya ukaguzi kwenye kikosi cha jeshi la anga, cha kituo cha uongozi cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) katika eneo la magharibi mwa China.

    Rais Xi amefanya ziara hiyo kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama na Kamati kuu ya kijeshi siku chache kabla ya Siku ya Jeshi la Ukombozi wa umma la China, ambayo huadhimishwa Agosti mosi, na kutoa salamu za dhati kwa maofisa na askari wote wa kituo cha uongozi cha jeshi la anga, pamoja na salamu za kuwatakia kila la heri kwa siku hiyo wafanyakazi wa PLA, vikosi vya polisi vya jeshi, wafanyakazi wa kiraia waliopo katika jeshi, mgambo na askari wa vikosi vya akiba.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha