<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Juzuu ya kwanza ya Kitabu cha Utawala wa China yazinduliwa Nairobi

    (CRI Online) Agosti 15, 2023

    (Picha inatoka CRI.)

    (Picha inatoka CRI.)

    Balozi wa China nchini Kenya Zhou Pingjian wakati wa uzinduzi wa juzuu ya kwanza ya kitabu cha Utawala wa China kilichoandikwa na Rais Xi Jinping, amesifia lugha ya Kiswahili na kuitaja kuwa daraja kati ya China na nchi zinazotumia lugha hii kwa mawasiliano.

    Balozi Zhou amesema kuwa kitabu hiki ni picha kamili ya ufanisi wa China.

    Hafla hii iliyoandaliwa katika Chuo Kikuu cha Nairobi, ilihudhuriwa na wageni mashuhuri wakiwemo, Waziri wa Utalii na Wanyapori wa Kenya Peninah Malonza, Waziri wa Utalii na Utamaduni wa China Hu Heping, Katibu Mkuu katika wizara ya Elimu kutoka idara ya Elimu ya Msingi, Paul Kibet, miongoni mwa wengine.

    Mgeni rasmi Waziri Malonza amesifu hatua hii ya kutafsiri kitabu cha Rais Xi kwa lugha ya Kiswahili, na kuitaja kuwa jukwaa la kuifanya Kenya kupata nguvu na hekima.

    “Katika safari yetu isiyo na kikomo katika mambo yanayotuleta pamoja, Kenya na China zimekuwa zikikumbatia tamaduni nyingi kutoka pande zote mbili. Tamaduni hizi zinawapa nguvu watu wetu na kuimarisha undugu na utamaduni.” Ameeleza.

    Akihutubia kwa niaba ya Waziri wa Elimu wa Kenya, Katibu Mkuu katika Idara ya Elimu ya Msingi, Paul Kibet amesema Kenya inaweza kuiga mambo mengi kutoka kwa China, namna ya kuinua kiwango cha elimu na haswa mtaala mpya wa CBC.

    “Nchi yetu inaweza ikaiga programu nyingi kutoka China. Kwa mfano, jinsi serikali ya watu wa China imeweza kuboresha kiwango chake cha elimu kwa mamilioni ya raia wake. Kuna mafunzo mengi tunayoweza kujifunza kutoka kwa kitabu cha Rais Xi Jinping. Tutazamie kujifunza na kutangamana mara kwa mara. ” amesema.

    Balozi wa China nchini Kenya Zhou Pingjian amesisitiza umuhimu na nguvu ya lugha katika mawasiliano. Ameongeza kuwa China inahitaji kujua mengi kuhusu dunia, kama dunia inavyozidi kujua mengi kuhusu China.

    “Juzuu nne za Xi Jinping zimefungua dirisha kwa jamii za kimataifa kuelewa China zaidi. Usomaji wa nakala ya kitabu hiki cha Utawala wa China kilichochapishwa kwa lugha ya Kiswahili nchini Kenya na kwingine kutawafanya watu kuelewa zaidi na kuona vyema jinsi China inavyojiendesha. Kwa niaba ya ubalozi wa China nchini Kenya, hapa Nairobi, napongeza idara ya uchapishashaji vitabu ya KLB na washirika wengine kwa uzinduzi wa juzuu ya kitabu hiki.” Amesema.

    Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya sera za Afrika profesa Peter Kagwanja ambaye alikuwa mmoja wa wageni waalikwa, amesema kitabu hiki kitawafaa siyo tu wananchi, bali pia viongozi wa nchi zinazozungumza Kiswahili.

    (Picha inatoka CRI.)

    (Picha inatoka CRI.)

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha