<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping wa China apokea nishani ya heshima ya juu ya Afrika Kusini

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 23, 2023

    Rais Xi Jinping wa China akipokea Nishani ya Afrika Kusini, ambayo ni ya ngazi ya juu zaidi na ya heshima ya juu zaidi ya Afrika Kusini kutoa kwa rais muhimu na rafiki wa nchi, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametoa nishani hiyo kwa Rais Xi baada ya mazungumzo yao huko Pretoria, Afrika Kusini, Agosti 22. 2023. Xi, ambaye anafanya ziara ya kiserikali nchini Afrika Kusini, amefanya mazungumzo na Ramaphosa siku ya Jumanne. (Xinhua/Yin Bogu)

    PRETORIA - Rais wa China Xi Jinping amepokea nishani ya Afrika Kusini kutoka kwa Rais Cyril Ramaphosa ambayo ni nishani ya ngazi ya juu zaidi na ya heshima ya juu zaidi ya Afrika Kusini kutoa kwa rais muhimu na rafiki wa nchi hiyo.

    Hafla ya kutoa nishani hiyo imefanyika Jumanne baada ya kumalizika mkutano kati ya Rais Xi na mwenzake Ramaphosa wakati wa ziara yake ya kiserikali nchini Afrika Kusini, na rais Xi pia atahudhuria Mkutano wa 15 wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS), na Xi na Rais Ramaphosa wataongoza pamoja Mazungumzo ya Viongozi wa China na Afrika.

    Akizungumza kwenye hafla hiyo, Rais Xi amesema ushirikiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Afrika Kusini umeingia katika "zama ya dhahabu," huku hali ya kuaminiana kisiasa kati ya pande hizo mbili ikiendelea kuongezeka, na ushirikiano wa kunufaishana na wa kufuata hali halisi katika sekta mbalimbali umepata matokeo yenye manufaa.

    “Nchi hizo mbili zimedumisha uratibu na ushirikiano wa karibu katika masuala ya kimataifa, jambo ambalo limekuza vyema maendeleo na ustawishaji wa nchi zao, na kutoa mchango zenye juhudi katika kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea,” amesema Rais Xi.

    Rais Xi amesisitiza kuwa haijalishi hali ya kimataifa itabadilika vipi, pande hizo mbili zitaendelea kujitolea katika kuimarisha urafiki na ushirikiano wa pande mbili.

    Huku akieleza kuwa atathamini heshima ya kupokea nishani ambayo ni ishara ya urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili, na ameahidi kusukuma mbele maendeleo endelevu ya uhusiano wa China na Afrika Kusini.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha