<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Bunge la Afrika Kusini lapongeza mafanikio ya Mkutano wa 15 wa Wakuu wa BRICS

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 28, 2023

    Watu wakitembea karibu na eneo la Mkutano wa 15 wa wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) huko Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 20, 2023. (Xinhua/Zhang Yudong)

    Watu wakitembea karibu na eneo la Mkutano wa 15 wa wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) huko Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 20, 2023. (Xinhua/Zhang Yudong)

    CAPE TOWN - Bunge la Afrika Kusini limetoa taarifa Jumamosi kuhusu mafanikio ya Mkutano wa 15 wa Wakuu wa Nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) uliofanyika Johannesburg, na kupongeza matokeo ya mkutano huu wa "kihistoria" kama "ushuhuda" wa uongozi wenye maono na dhamira isiyoyumba ya nchi za BRICS.

    "Matokeo ya Mkutano wa 15 wa BRICS yanajumuisha moyo wa ushirikiano wa kimataifa wenye nguvu, unaosisitiza ushirikiano wa pande nyingi, utatuzi wa migogoro kwa amani, na kutafuta maendeleo endelevu," imesema taarifa hiyo.

    Rais Xi Jinping wa China, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Mkutano wa 15 wa Wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 23. 2023. (Xinhua/Li Xueren)

    Rais Xi Jinping wa China, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Mkutano wa 15 wa Wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini (BRICS) mjini Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 23, 2023. (Xinhua/Li Xueren)

    Imesema kuwa mkutano huo umeshughulikia ukosefu wa usawa wa kiuchumi, kuhimiza ukuaji wa uchumi na kutafuta utatuzi wenye uvumbuzi wa kifedha, jambo ambalo linatoa matumaini kwa nchi za BRICS bali pia ni chanzo cha maendeleo na utulivu kwa Afrika na Dunia nzima.

    "Kwa kutetea mageuzi ya kifedha duniani, kuhimiza mabadilishano kati ya watu na kutetea mahitaji ya nchi za Kusini, mkutano huo unaweka kielelezo cha maendeleo yenye usawa, uelewa wa kitamaduni na ushirikiano jumuishi ambao unalenga kuinua uchumi, kuimarisha ushirikiano na kuweka mazingira ya kimataifa yenye masikilizano," inasomeka taarifa hiyo.

    Katika taarifa hiyo, Bunge la Afrika Kusini pia limepongeza uamuzi wa pamoja wa kupanua kundi la BRICS kwa kuzikaribisha nchi wanachama wapya ambazo ni Saudi Arabia, Iran, Ethiopia, Misri, Argentina na Umoja wa Falme za Kiarabu.

    Rais Xi Jinping wa China akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine waliohudhuria Mazungumzo ya nchi za BRICS na Afrika na BRICS Plus huko Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 24, 2023. (Xinhua/Li Xueren)

    Rais Xi Jinping wa China akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine waliohudhuria Mazungumzo ya nchi za BRICS na Afrika na BRICS Plus huko Johannesburg, Afrika Kusini, Agosti 24, 2023. (Xinhua/Li Xueren)

    "Upanuzi huu unaashiria kujitolea kwa BRICS kwa ujumuishi, mirengo tofauti na maendeleo ya pamoja. Manufaa ya upanuzi huu yanaenea siyo tu barani Afrika bali yanafika kimataifa, hasa kwa nchi zinazoendelea, zenye masoko yanayoibukia, na kuhimiza ujenzi wa Dunia yenye ncha nyingi," imesema taarifa hiyo.

    Kupanuka kwa BRICS kunawakilisha hatua ya kimkakati kuelekea kukuza maendeleo ya ushirikiano, uvumbuzi na uimarishaji wa uhusiano wa kiuchumi," imesema taarifa hiyo. "Ujumuishaji wa nchi wanachama wapya unaleta fursa mpya za kutumia nguvu za pamoja ili kukabiliana na tofauti za kiuchumi, kukuza ukuaji endelevu wa uchumi, na kuongeza sauti za nchi zinazoendelea katika jukwaa la kimataifa."

    (Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

    Picha