<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping aagiza juhudi za pande zote za uokoaji na uchunguzi wa kina kuhusu maafa ya mafuriko katika Mkoa wa Sichuan

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 31, 2023

    BEIJING - Rais Xi Jinping wa China ameagiza kufanya juhudi za pande zote za kuwatafuta na kuwaokoa watu wote ambao hawajulikani walipo kutokana na maafa ya mafuriko yaliyotokea hivi majuzi katika Mkoa wa Sichuan, Kusini-Magharibi mwa China.

    Rais Xi pia ametaka kufanya uchunguzi wa kina na kuimarisha usimamizi wa usalama ili kuhakikisha usalama wa maisha na mali za watu.

    Kipindi kifupi cha mvua kubwa iliyonyesha Agosti 21 imesababisha maafa katika eneo la ujenzi wa barabara kuu kando ya mto katika Wilaya ya Jinyang iliyoko Eneo linalojiendesha la Kabila la Wayi la Liangshan mkoani Sichuan.

    Katika maagizo yake, Rais Xi ametoa wito wa kuhakikisha hatua zinazofaa kwa ajili ya kufariji familia za waathiriwa.

    Amelitaka Baraza la Serikali la China kutuma kikosi kazi kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kina wa maafa hayo na kuwachukulia hatua kali waliohusika kwa mujibu wa sheria.

    “Lazima kujifunza kutokana na maafa na kufanya ukaguzi wa kina ili kushughulikia matatizo na hatari na kuhakikisha kwamba pande zote zinazohusika zinatekeleza wajibu wao,” Rais Xi amesema.

    Waziri Mkuu wa China Li Qiang pia ametoa agizo, akihimiza kubaini ukweli na habari muhimu haraka iwezavyo, pamoja na kufanya juhudi ziwezavyo za kutafuta na kuokoa watu ambao hawajulikani walipo.

    Kufuatia maagizo kutoka kwa Rais Xi na Waziri Mkuu Li, Wizara ya Usimamizi wa Dharura ya China imetuma kikundi kazi kwenye eneo la maafa ili kusimamia shughuli za uokoaji na utafutaji wa watu.

    Serikali ya Mkoa wa Sichuan na Wilaya ya Liangshan pia zinakusanya vikosi vya uokoaji kwa ajili ya kazi ya uokoaji.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha