<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping aongoza ufunguaji mlango wa sekta ya huduma ya China?na?ushirikiano ili kusukuma ufufukaji wa?Uchumi wa Dunia

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 04, 2023

    Rais Xi Jinping wa China akihutubia Mkutano wa Kilele wa Biashara ya Huduma ya Kimataifa wa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China ya Mwaka 2023 (CIFTIS) kwa njia ya video mjini Beijing, China, Septemba 2, 2023. (Xinhua/Li Xueren)

    Beijing - Rais Xi Jinping wa China amehutubia Mkutano wa Kilele wa Biashara ya Huduma ya Kimataifa wa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China ya Mwaka 2023 (CIFTIS), na kuipeleka nchi ya China yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani kupiga hatua zaidi katika kufungua sekta yake ya huduma na kuimarisha ushirikiano ili kusukuma ufufukaji wa uchumi wa Dunia.

    "Dunia leo inakabiliwa na mabadiliko ya kasi ambayo hayajawahi kuonekana katika karne moja iliyopita na ufufukaji goigoi wa uchumi," Rais Xi amesema katika hotuba yake siku ya Jumamosi asubuhi kwa njia ya video.

    Amesisitiza umuhimu wa biashara ya huduma ni sehemu muhimu ya biashara ya kimataifa, akisisitiza jukumu muhimu la sekta ya huduma katika ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi mbalimbali.

    Ameeleza kwamba ushirikiano wa kimataifa katika biashara ya huduma na sekta ya huduma umeimarishwa, mchakato wa ukuaji wa uchumi unaoendeshwa kidijitali, kwa teknolojia za kisasa na ulio rafiki kwa mazingira umeharakishwa, na teknolojia mpya pamoja na aina na miundo mipya ya biashara umekua, hayo yametoa msukumo mkubwa katika kuendeleza utandawazi wa kiuchumi, kuimarisha uhai wa uchumi wa kimataifa na kuwezesha uthabiti wa maendeleo ya uchumi wa Dunia.

    Akibainisha kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya mwaka wa 45 tangu China ianzishe sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, Rais Xi amesisitiza dhamira ya nchi hiyo ya kuendeleza ufunguaji mlango wa kiwango cha juu na kuendeleza maendeleo ya kisasa ya China katika sekta zote kupitia maendeleo yenye ubora wa juu, na hivyo kuzipa nchi zote fursa mpya za kufungua mlango na kufanya ushirikiano.

    Rais Xi ametaja hatua mbalimbali za kuweka mazingira ya maendeleo yaliyo "wazi zaidi na shirikishi zaidi", ambazo ni pamoja na kupanua mtandao wa maeneo ya biashara huria yenye kiwango cha juu kwa kulenga dunia nzima, kufanya mazungumzo juu ya orodha hasi ya biashara ya huduma na uwekezaji, na kufungua mlango zaidi katika maeneo ya huduma kama vile mawasiliano ya simu, utalii, sheria na tathmini ya ujuzi wa kiufundi katika ufanisi kazini.

    Juu ya suala la ushirikiano, Rais Xi amesema China itaimarisha uhusiano na ushirikiano wa kunufaishana kwa kuimarisha muunganisho wa mikakati ya maendeleo na mipango ya ushirikiano kati ya nchi mbalimbali, kuimarisha ushirikiano wa biashara za huduma na biashara za kidijitali na nchi washirika wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kurahisisha rasilimali na mambo ya uzalishaji kuvuka mipaka na kupanua maeneo zaidi ya ukuaji wa ushirikiano wa kiuchumi.

    Maonyesho ya CIFTIS ya Mwaka 2023 yanafanyika Beijing kuanzia Jumamosi hadi Jumatano yakiwa na kaulimbiu ya "Ufunguaji mlango unaongoza maendeleo, ushirikiano wa kunufaishana unaleta siku zijazo."

    Rais Xi Jinping wa China akihutubia Mkutano wa Kilele wa Biashara ya Huduma ya Kimataifa wa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China ya Mwaka 2023 (CIFTIS) kwa njia ya video mjini Beijing, China, Septemba 2, 2023. (Xinhua/Li Xueren)

    Rais Xi Jinping wa China akihutubia Mkutano wa Kilele wa Biashara ya Huduma ya Kimataifa wa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China ya Mwaka 2023 (CIFTIS) kwa njia ya video mjini Beijing, China, Septemba 2, 2023. (Xinhua/Li Xueren)

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha