<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    China na Benin zaanzisha ushirikiano wa kimkakati

    (CRI Online) Septemba 04, 2023

    (Picha inatoka Xinhua.)

    (Picha inatoka Xinhua.)

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Benin Patrice Athanase Guillaume Talon, wametangaza kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi zao.

    Hatua hiyo imetangazwa baada ya kufanyika kwa mazungumzo kati ya Rais Xi na Rais Talon, ambaye yuko ziarani nchini China.

    Kwenye mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye jumba la mikutano ya umma hapa Beijing, China Rais Xi amebainisha kuwa katika miaka ya hivi karibuni uhusiano kati ya China na Benin umekuwa na maendeleo ya kasi, na maendeleo madhubuti yamepatikana katika ushirikiano wa kivitendo.

    Ameongeza kuwa nchi hizo mbili zimesaidiana kwenye masuala yanayohusiana na maslahi ya kimsingi ya kila upande na yale yanayofuatiliwa sana, na kudumisha mawasiliano na uratibu madhubuti katika mambo ya kimataifa.

    Rais Xi amesisitiza kuwa China inashikilia umuhimu wa kuendeleza uhusiano kati yake na Benin, na iko tayari kudumisha mabadilishano katika ngazi zote, kuhimiza ushirikiano wa kirafiki na wenye faida katika nyanja mbali mbali, na kufikisha uhusiano wa nchi mbili kwenye kiwango kipya.

    (Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

    Picha