<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping atuma barua ya pongezi kwa Maonyesho ya Teknolojia za Kisasa ya China

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 05, 2023

    BEIJING – Rais wa China Xi Jinping ametuma barua ya pongezi kwa Maonyesho ya Teknolojia za Kisasa ya China Mwaka 2023 (Smart China Expo 2023), ambayo yamefunguliwa Jumatatu katika mji wa Chongqing, Kusini Magharibi mwa China.

    Rais Xi amesema katika barua hiyo kwamba teknolojia za kisasa kama vile intaneti, data kubwa, kompyuta ya wingu, teknolojia za akili bandia na blockchain zinapitia mabadiliko makubwa; mageuzi ya kidijitali, ya teknolojia za akili bandia na yaliyo rafiki kwa mazingira yanaongezeka kwa kasi; na sekta ya akili bandia na uchumi wa kidijitali vinastawi. Amesema, haya yamebadilisha sana mgawanyo wa kimataifa wa vipengele vya uzalishaji na rasilimali katika uchumi, njia ya kuendeleza viwanda, na mitindo ya maisha ya watu.

    Rais Xi amesema China inatilia maanani sana maendeleo ya uchumi wa kidijitali, China inaendelea kuhimiza mafungamano ya pande zote ya teknolojia za kidijitali na uchumi halisi, kuratibu maendeleo katika viwanda vya kutoa teknolojia za kidijitali na mageuzi ya kidijitali ya viwanda vya kijadi, na kuharakisha ujenzi wa nguvu ya mtandao na kuifanya China kuwa ya kidijitali.

    “China iko tayari kufanya kazi na nchi mbalimbali duniani ili kuchukua fursa ya mwelekeo mpya wa zama ya kidijitali, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa katika nyanja ya kidijitali, kuchochea uvumbuzi na maendeleo katika sekta ya teknolojia za akili bandia, kuharakisha ujenzi wa jumuiya ya mtandao yenye mustakabali wa pamoja, na kufanya kazi pamoja kujenga mustakabali mzuri zaidi,” Rais Xi amesema katika barua hiyo.

    Yakiwa na kaulimbiu isemayo “Kuunganisha Pamoja Hekima na Nguvu," maonyesho hayo yamepangwa kufanyika hadi Jumatano wiki hii.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha