Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping wa China akutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu Mirjana Spoljaric Egger kwenye Jumba la Mikutano ya Umma hapa Beijing, China, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) Mirjana Spoljaric Egger mjini Beijing siku ya Jumanne.
Rais Xi amepongeza kazi ya kimataifa ya huduma za ubinadamu iliyofanywa na ICRC katika miaka 160 iliyopita tangu kuanzishwa kwake na kupongeza mchango wake muhimu kwa amani na maendeleo ya Dunia.
Rais Xi ameeleza kuwa Dunia leo inapitia mabadiliko makubwa ambayo hayajapata kutokea katika karne moja iliyopita, na jamii ya binadamu inakabiliwa na changamoto nyingi, ambazo baadhi yake ni za kawaida na baadhi ni mpya. Amesema, chini ya hali hiyo, China inaimarisha ushirikiano na nchi nyingine ili kutafuta suluhu kwa pamoja na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
"Nilitoa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia kwa matumaini ya kushirikiana na nchi zingine kufikia maendeleo ya kiuchumi, kuboresha maisha ya watu, kupata matokeo yenye manufaa kwa pande zote, na kutoa mawazo na suluhu za China kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa Dunia na usimamizi wa masuala kuhusu ubinadamu ," Rais Xi amesema.
Akiuita ubinadamu kuwa maafikiano makubwa zaidi yanayoweza kuunganisha ustaarabu tofauti, Rais Xi amesema mawazo yaliyomo katika utamaduni wa kijadi wa China kama vile "mtu mwema anapenda wengine" na “usiwatendee wengine usichotaka kutendewa” yanashabihiana na nia ya Harakati za Kimataifa za Msalaba Mwekundu.
“Kwa kutilia maanani kanuni ya kuwaweka watu kwenye kipaumbele cha juu, China imeshinda vita kubwa zaidi dhidi ya umaskini katika historia ya binadamu. Katika kukabiliana na UVIKO-19, China haijalinda tu maisha na afya ya watu wake bali pia imetoa msaada mkubwa zaidi wa kibinadamu duniani katika historia,” Rais Xi amesema.
Kwa upande wake, Spoljaric ameipongeza China kwa kuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya wapokeaji wa Tuzo ya 49 ya Florence Nightingale, jambo ambalo linaonyesha kuwa ICRC na jumuiya ya kimataifa zinatambua sana mafanikio ya China katika mambo ya ubinadamu.
Amesema China daima imekuwa ikiheshimu na kutekeleza sheria za kimataifa za ubinadamu, na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja limesaidia maendeleo ya Dunia na kuendeleza mambo ya ubinadamu duniani.
Rais Xi Jinping wa China akikutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu Mirjana Spoljaric Egger kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Septemba 5, 2023. (Xinhua/Ding Lin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma