Lugha Nyingine
Washindi wa Fainali za Mashindano ya Kimataifa ya “Simulizi yangu ya maandishi ya Kichina Hanzi” kwa Mwaka 2023 Wateuliwa
Mashindano ya Kimataifa ya “Simulizi yangu ya maandishi ya kichina Hanzi” kwa mwaka wa 2023, ambayo yanaandaliwa na Shirika la Urafiki wa Watu wa China kwa Watu wa Nje na kuendeshwa na Tovuti ya Gazeti la Umma yataingia fainali, baada ya duru mbili za awali na nusu fainali za mashindano kufanyika.
Mwaka 2023 umekuwa mwaka wa 10 tangu kutolewa kwa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Mashindano hayo yana kaulimbiu ya “Maskani ”, yakiwaalika watu kutoka nchi mbalimbali kutoa simulizi zao kuhusu kufundishana na kuelewana kati ya ustaarabu mbalimbali . Mashindano hayo yanagawanywa katika hatua tatu za awali, nusu fainali na fainali. Timu 10 ya washindi waliofanya vizuri zaidi katika nusu fainali walichaguliwa tena na kamati ya maandalizi kuendelea kwenye mashindano ya hatua ya fainali
Fainali ya mashindano imepangwa kufanyika Tarehe 14, Septemba, 2023 katika Mji wa Jincheng, Mkoa wa Shanxi, China, ambapo kila mshiriki wa fainali atatoa hotuba ya dakika 7 kwa kufuata kaulimbiu ya “Maskani ”. Tuzo mbalimbali zitatangazwa baada ya kuzingatia alama na tathimini ya mwisho kufanywa na waamuzi wa mashindano.
Orodha ya majina ya washiriki wa fainali (yameorodheshwa kwa kufuata utaratibu wa herufi ya kwanza kwenye alfabeti ya jina la nchi ya kila mshiriki )
1. Yasser Mahamad Senoussi+Ousama Mahamad Senoussi Ahmad, Chad, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia ya Elektroniki
2. Moses Arthur Baidoo, Ghana, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Donghua
3.Lydia Nduta Njoroge, Kenya, Chuo Kikuu cha Ualimu cha Qufu
4.Senyord Chanmaly, Laos, Chuo Kikuu cha Shanxi
5.Oyungerel Gegee, Mongolia, Chuo Kikuu cha Mongolia ya Ndani
6.Ojimmadu Raphael Ebube, Nigeria, Chuo Kikuu cha Lugha za Kigeni cha Shanghai
7.Kaleem Sajid, Pakistan
8.Ratajczak Paulina Magdalena, Poland, Chuo cha Ualimu cha Anshan
9. Siniakov Andrei,? Russia, Chuo Kikuu cha Ufundi wa Viwanda cha Yancheng
10.Sejoud Isam Mahir Hassan, Sudan, Chuo Kikuu cha Lanzhou
Mpango wa Tuzo za Washindi :
Fainali itatoa tuzo maalum kwa Mshindi mmoja;
Washindi wawili wa Nafasi ya Kwanza ya Tuzo;
Washindi watatu wa Nafasi ya Pili ya Tuzo ;
Washindi wanne wa Nafasi ya Tatu ya Tuzo;
Mashindano kwenye eneo la ng’ambo yatakuwa na mshindi wa Tuzo maalumu ya Bingwa.
Kila mshindi atapata cheti, zawadi ya kumbukumbu ya mji mwenyeji na zawadi ya pesa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma