Lugha Nyingine
Maonyesho ya utamaduni wa China yafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU)
Msanii wa kundi la Opera ya Wu la Zhejiang akifanya maonesho ya mchezo wa sanaa wa Opera ya Wu ya "Ushindi mara tatu dhidi ya jini mifupa" kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia, Septemba 8, 2023. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)
ADDIS ABABA - Maonesho ya utamaduni wa China yamefanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa siku ya Ijumaa kufanya hafla ya pamoja ya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Shirikisho la Umoja wa Afrika (OAU), kwa sasa ni Umoja wa Afrika AU, na Siku ya AU.
Katika shughuli za maonesho hayo, wasanii 30 wa opera wa China waliwasilisha maonyesho ya michezo ya sanaa jukwaani kwa wageni pamoja na maonyesho ya mavazi na vifaa vya opera ya Kichina pamoja na vinyago vya mbao vya China na Sanaa ya ukataji karatasi. Maonyesho ya sanaa ya sarakasi na Kung Fu pia yalifanyika.
Mkuu wa ujumbe wa China kwenye Umoja wa Afrika, Hu Changchun amesema katika miaka ya hivi karibuni China na Afrika zimekuwa na mawasiliano ya kitamaduni na mawasiliano kati ya watu yenye nguvu, ambayo yanachangia uhusiano wa jumla wa China na Afrika.
"China na Afrika ni chimbuko la ustaarabu, zikiwa na historia, utamaduni na urithi wa kisanii wa ajabu unaothaminiwa kwa muda mrefu. Ustaarabu wetu umekuwa na nafasi kubwa katika kustawi kwa maendeleo ya binadamu na Dunia," amesema.
Albert Muchanga, Kamishna wa AU wa Maendeleo ya Uchumi, Biashara, Utalii, Viwanda na Madini, akihutubia amesisitiza haja ya kuimarisha uhusiano wa pande zote kati ya China na Afrika chini ya mwavuli chombo cha bara hilo, AU.
Wageni waliofurahia maonyesho ya utamaduni wa China pia wamesisitiza haja ya kuimarisha uhusiano wa utamaduni kati ya watu wa pande hizo mbili ili kuimarisha ushirikiano unaoendelea kukua.
Maonyesho hayo ya utamaduni wa China yameandaliwa kwa pamoja na Ujumbe wa China kwa AU na Kamisheni ya AU, yakihusisha sanaa ya kijadi na maonyesho ya michezo ya Sanaa ya opera ya kijadi ya China pamoja na maonyesho mengine ya jukwaani.
Msanii wa kundi la Opera ya Wu la Zhejiang akionesha na kuimba Opera ya Wu ya "Binti wa Mbinguni Anayetawanya Maua" kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Ethiopia, Septemba 8, 2023. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma