Lugha Nyingine
Ujerumani yashinda Kombe la Dunia la Mpira wa Kikapu la FIBA kwa mara ya kwanza katika historia
Timu ya Taifa ya Ujerumani ikisherehekea kushinda Fainali ya Kombe la Dunia la Mpira wa Kikapu la FIBA mjini Manila, Ufilipino, Septemba 10, 2023. (Xinhua/Meng Yongmin)
MANILA - Ujerumani imeipiga Serbia pointi 83-77 na kunyakua taji lake la kwanza la Kombe la Dunia la Mpira wa Kikapu la FIBA Jumapili jioni huku mchezaji wake kinara Dennis Schroder akitajwa kuwa Mchezaji wa Thamani Zaidi (MVP) wa mashindano hayo.
Schroder, akijivunia wastani wa pointi 17.6, kutoa msaada kwa wastani 6.1, na ukabaji wa mipira kutoka kwa timu pinzani mara mbili katika muda wote wa Kombe la Dunia, alifikisha pointi 28 katika mchezo huo wa fainali. Franz Wagner alichangia pointi 19 na ukabaji wa mipira kutoka kwa timu pinzani mara saba, huku Johannes Voigtmann akiongeza pointi 12 na ukabaji mipira kutoka kwa timu pinzani mara saba.
Dennis Schroder (Kulia) wa Ujerumani akifunga kikapu katika mchezo wa fainali dhidi ya Serbia kwenye Kombe la Dunia la Mpira wa Kikapu la FIBA 2023 mjini Manila, Ufilipino, Septemba 10, 2023. (Xinhua/Wu Zhuang)
Kwa Serbia, Aleksa Avramovic aliongoza kwa kupachika vikapu vingi akiwa na pointi 21, naye Bogdan Bogdanovic aliingia akiwa na pointi 17 na kutoa msaada mara tano. Nikola Milutinov, hata hivyo, alitatizika, akikosa majaribio yake yote manne na kumaliza mchezo akiwa na alama mbili pekee na kutoa msaada mara nne.
Uwanja wa The Mall of Asia ulikuwa ni kama uwanja wa nyumbani kwa Serbia, kutokana kushangiliwa sana na mashabiki wao. Hata hivyo, mashaka ya ushindi yalianza mapema wakati Ognjen Dobric alipopata jeraha na kulazimika kutoka nje ya uwanja dakika tatu tu baada ya mchezo kuanza.
Kihistoria, katika kila fainali tano zilizopita za mashindano haya, timu inayoongoza hadi wakati wa mapumziko iliibuka mshindi. Lakini fainali ya Jumapili ilishuhudia timu zote zikiwa zimefungana kwa pointi 47 wakati wa mapumziko.
Daniel Theis (Kushoto) wa Ujerumani akipoteza uwiano wa mwili katika mchezo wa fainali dhidi ya Serbia kwenye Kombe la Dunia la Mpira wa Kikapu la FIBA 2023 huko Manila, Ufilipino, Septemba 10, 2023. (Xinhua/Wu Zhuang)
Dennis Schroder (wa pili kushoto) wa Ujerumani akijiweka sawa kufunga kikapu katika mchezo wa fainali dhidi ya Serbia kwenye Kombe la Dunia la Mpira wa Kikapu la FIBA 2023 mjini Manila, Ufilipino, Septemba 10, 2023. (Xinhua/Wu Zhuang)
Schroder, akionyesha ustahimilivu chini ya shinikizo, alipanga shambulizi ambalo lilisababisha adhabu na akarusha mipira miwili ya adhabu na kufunga vikapu viwilil ambavyo viliihakikishia ushindi Ujerumani.
Ujerumani haikupoteza mchezo hata mmoja na kushinda michezo yote minane, na kuwa nchi ya nne ya Ulaya na ya saba kwa jumla kushinda taji la dunia. Pia imekuwa ni mara ya kwanza kwa Ujerumani kutwaa taji la Kombe la Dunia la FIBA baada ya kuingia kwa mara ya kwanza hatua ya fainali, tangu Hispania ilipofanya hivyo kwa kumenyana na Ugiriki Mwaka 2006.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma