<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping atuma barua ya pongezi kwa Kongamano la Utamaduni la Beijing Mwaka?2023

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 15, 2023

    BEIJING - Rais Xi Jinping leo Alhamisi ametuma barua ya pongezi kwa Baraza la Utamaduni la Beijing Mwaka 2023 lililofunguliwa mapema leo mjini Beijing.

    Katika barua yake hiyo, Rais Xi amedhihirisha kuwa, Taifa la China lina utamaduni bora wa jadi wenye historia ndefu, ambao tangu enzi na Dahari umekumbatia uwazi na ujumuishaji, na tangu zamani za kale ustaarabu wa Taifa la China umethamini hali ya kuelewana na kuheshimiana kati ya ustaarabu mbalimbali tofauti.

    Amesema, "Beijing imekuwa na historia ndefu na urithi mkubwa wa kitamaduni, ni ushuhuda wenye nguvu juu ya mwendelezo, uvumbuzi, umoja, ujumuishaji na asili ya amani ya ustaarabu wa Taifa la China".

    Amesema China itatumia nguvu bora ya Beijing iliyokuwa mji mkuu wa kale na kituo cha utamaduni cha kitaifa ili kuimarisha mawasiliano ya kitamaduni na sehemu mbalimbali duniani, ili kuhimiza kwa pamoja ustawi na maendeleo ya utamadunia, uhifadhi wa urithi wa utamadunia, kufanya mawasiliano na kufundishana kati ya ustaarabu na kutekeleza Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia, na kutia nguvu kubwa ya utamaduni iliyo ya kudumu kwa ajili ya kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Baraza hilo lenye kaulimbiu isemayo “kurithisha utamaduni bora na kuhimiza mawasiliano na ushirikiano", limeandaliwa kwa pamoja na Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Kamati ya Chama ya Mji wa Beijing na Serikali ya Mji wa Beijing.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha