<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping atoa wito wa muunganisho bora wa mchakato wa maendeleo ya kisasa kati ya China na Singapore

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 15, 2023

    Beijing - Rais wa China Xi Jinping amesema yuko tayari kufanya ushirikiano na Rais wa Singapore Tharman Shanmugaratnam katika kuhimiza hali ya kuunganishwa vizuri zaidi na kuboreshana kwa mchakato wa maendeleo ya kisasa nchini China na Singapore.

    Rais Xi ametoa wito huo Alhamisi katika salamu zake za pongezi kwa Tharman Shanmugaratnam kwa kuchukua wadhifa wake wa kuwa rais wa Singapore.

    Rais Xi amesema kuwa China na Singapore, kila upande ni jirani wa kirafiki na mshirika muhimu wa ushirikiano kwa upande mwingine, kwa juhudi za pande zote mbili, China na Singapore kwa pamoja zimeweka mkondo wa mafanikio unaojumuisha kufundishana na kufanya ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote, jambo ambalo linatia msukumo wenye nguvu kwa maendeleo na ustawishaji wao wa kitaifa, na pia kuweka mfano wa ushirikiano kati ya nchi katika kanda.

    Rais Xi amesema mwaka huu, uhusiano kati ya China na Singapore umeinuliwa na kufikia ushirikiano wa pande zote wenye mwelekeo wa kiwango cha juu katika siku zijazo, na kuweka mkondo wa maendeleo yenye ubora wa juu ya uhusiano wa nchi hizo mbili katika zama mpya.

    Rais wa China amesema anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Singapore na yuko tayari kuanzisha uhusiano mzuri wa kikazi na Tharman Shanmugaratnam ili kuleta uhusiano kati ya China na Singapore katika ngazi mpya, kuhimiza hali ya kuunganisha na kukamilisha vizuri kwa mchakato wa maendeleo ya kisasa wa pande hizo mbili, ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa pande mbili na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya amani, ustawi na utulivu wa kikanda.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha