<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping afungua michezo mikubwa zaidi ya Asia, akitetea amani, mshikamano na ujumuishaji

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 25, 2023

    Rais wa China Xi Jinping akipunga mkono kwenye sherehe za  kufunguliwa kwa Michezo ya 19 ya Asia huko Hangzhou, Mji Mkuu wa Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Septemba 23, 2023. (Xinhua/Yue Yuewei)

    Rais wa China Xi Jinping akipunga mkono kwenye sherehe za kufunguliwa kwa Michezo ya 19 ya Asia huko Hangzhou, Mji Mkuu wa Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Septemba 23, 2023. (Xinhua/Yue Yuewei)

    HANGZHOU - Chini ya miaka miwili baada ya kufanyika kwa mafanikio Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumamosi amefungua Michezo ya Asia ya Hangzhou, ambayo ni mikubwa zaidi kwa kuwa na ushiriki wa wanamichezo na shughuli za michezo katika historia ya miaka 72 tangu kuanza kwa michezo hiyo.

    "Ninatangaza kuwa Michezo ya 19 ya Asia imefunguliwa," Rais Xi amesema kwa sauti yake nzito na yenye nguvu kwenye uwanja mkubwa wenye viti vya kukaa kwa watu zaidi ya 80,000 huko Hangzhou, mji wenye mandhari nzuri ambapo uliwahi kusifiwa na msafiri wa Kiitaliano wa Karne ya 13 Marco Polo kama "Mji wa Mbinguni, ulio bora zaidi na mtukufu zaidi duniani."

    Michezo hiyo, iliyofunguliwa katika Uwanja wa Kituo cha Michezo cha Olimpiki cha Hangzhou wenye umbo la maua ya yungiyungi, ulikuwa umejaa wanamichezo zaidi ya 12,000 kutoka pande wanachama wote 45 wa Baraza la Olimpiki la Asia (OCA), ambao watashindana kwenye michezo 481 katika aina 40 za michezo.

    Michezo ya Asia ya Hangzhou ni ya tatu ya kufanyika nchini China, baada ya Beijing 1990 na Guangzhou 2010.

    Viongozi wa kigeni walioungana na Rais Xi katika sherehe hizo ni pamoja na Mfalme Norodom Sihamoni wa Cambodia, Rais Bashar al-Assad wa Syria, Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach, na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Asia Raja Randhir Singh.

    Mbali na shughuli za gwaride la wanamichezo, utoaji hotuba na maonyesho ya kuvutia kwenye sherehe za kufunguliwa kwa Michezo ya Asia, watazamaji pia walishuhudia maonesho ya kipekee ikiwa ni pamoja na fashifashi za kidijitali na kikimbiza mwenge cha kidijitali, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Hangzhou kufanya michezo hiyo kuwa yenye kutumia teknolojia za akili bandia bila kutoa uchafuzi kwa mazingira.

    Wang Shun na kikimbiza mwenge cha kidijitali kwa pamoja wakiwasha chombo kikubwa cha chuma kwenye sherehe ya kufunguliwa kwa Michezo ya 19 ya Asia huko Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Septemba 23, 2023. (Xinhua/Jiang Han)

    Wang Shun na kikimbiza mwenge cha kidijitali kwa pamoja wakiwasha chombo kikubwa cha chuma kwenye sherehe ya kufunguliwa kwa Michezo ya 19 ya Asia huko Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Septemba 23, 2023. (Xinhua/Jiang Han)

    Rais Xi ni mtetezi mkubwa wa michezo, na hutupia macho yake zaidi ya Michezo.

    Yeye na viongozi mbalimbali wa kigeni walifanya mikutano mingi ya pande mbili mbili katika siku kadhaa zilizopita kabla ya kufunguliwa kwa michezo hiyo, ambapo walijadili masuala mbalimbali. Rais Xi na Assad wametangaza kuanzisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Syria. Rais Xi na Waziri Mkuu Xanana Gusmao wa Timor-Leste wametangaza kupandisha uhusiano wa pande mbili uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote.

    Akihutubia karamu ya kuwakaribisha viongozi hao kabla ya kufunguliwa kwa michezo hiyo, Rais Xi ametoa wito wa kutumia nafasi ya michezo ili kuhimiza amani, mshikamano na ujumuishaji.

    Wasanii  wakifanya maonesho kwenye sherehe za kufunguliwa kwa Michezo ya 19 ya Asia huko Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Septemba 23, 2023. (Xinhua/Jiang Wenyao)

    Wasanii wakifanya maonesho kwenye sherehe za kufunguliwa kwa Michezo ya 19 ya Asia huko Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Septemba 23, 2023. (Xinhua/Jiang Wenyao)

    "Tunapaswa kutumia michezo kuhimiza amani, kutafuta ujirani mwema na kunufaishana, na kukataa mawazo ya Vita Baridi na mapambano ya kambi," Rais Xi amewaambia wageni. "Tunapaswa kuifanya Asia kuwa nguzo muhimu ya amani duniani."

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha