<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping asisitiza kushiriki kwa juhudi katika mageuzi ya WTO na kuongeza uwezo wa kufungua mlango kwenye kiwango cha juu

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 28, 2023

    BEIJING – Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesisitiza kufanya juhudi za kushiriki kikamilifu katika mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani (WTO) na kuongeza uwezo wa kufungua mlango kwenye kiwango cha juu wa China.

    Rais Xi ameyasema hayo alipokuwa akiongoza semina elekezi ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC Jumatano.

    Rais Xi amesema kuwa, WTO ni nguzo muhimu ya ushirikiano wa pande nyingi na jukwaa muhimu la usimamizi wa uchumi wa Dunia, ni makubaliano ya pamoja na mwelekeo wa jumla wa kutekeleza mageuzi muhimu ya WTO.

    Amehimiza kufanya juhudi za China kushiriki kikamilifu katika mageuzi ya WTO na marekebisho ya kanuni za uchumi na biashara za kimataifa, kufungua mlango kwenye kiwango cha juu ili kuhimiza mageuzi ya kina na maendeleo ya ubora wa juu ya China .

    “Tangu ilipojiunga na WTO miaka zaidi ya 20 iliyopita, China imekuwa mfanyabiashara mkubwa zaidi wa bidhaa duniani na mshirika mkuu wa biashara kwa zaidi ya nchi na kanda 140, na kuchangia wastani wa karibu asilimia 30 katika ukuaji wa uchumi wa Dunia kwa mwaka,” Rais Xi amesema.

    Rais Xi amesema, Mabadiliko ya kihistoria yametokea katika uhusiano kati ya China na WTO, China imekua hatua kwa hatua kutoka kuwa mpokeaji na mpitishaji tu wa kanuni za uchumi na biashara za kimataifa , hadi kuwa mshiriki muhimu katika nyanja hii.

    Amesema, ukweli umethibitisha kwamba uamuzi wa China kujiunga na WTO umekuwa sahihi kabisa, kwani kujiunga nayo siyo tu kumeharakisha maendeleo ya China yenyewe bali pia kunanufaisha Dunia nzima.

    Kuhusu kushiriki katika mageuzi ya WTO, Rais Xi ametoa wito wa kutilia maanani kwa uthabiti mamlaka na ufanisi wa mfumo wa biashara wa pande nyingi huku WTO ikiwa kiongozi, na kuhimiza kikamilifu kurejeshwa kwa utendaji na ufanisi wa kawaida wa utaratibu wa utatuzi wa migogoro wa WTO.

    Amesisitiza haja ya China kushikamana na mwelekeo wa jumla wa utandawazi wa uchumi, kutetea biashara huria na ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, kupinga msimamo wa upande mmoja na kujihami kibiashara, kupinga kuingiza siasa, kuitumia kama silaha na kuongeza maana ya usalama kuhusu masuala ya uchumi na biashara, na kujenga uchumi wa Dunia ulio wazi.

    Rais Xi ameeleza kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 45 tangu China ianze mageuzi na kufungua mlango, na amehimiza kufanya juhudi za kufungulia mlango nchi za nje na kupiga hatua thabiti katika mageuzi.

    (Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

    Picha