<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping ampongeza Muizzu kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Maldives

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 05, 2023

    BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma salamu za pongezi kwa Mohamed Muizzu kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Maldives.

    Kwenye salamu zake hizo alizozituma siku ya Jumanne, Rais Xi amesema kuwa China na Maldives zinafurahia historia ndefu ya mabadilishano ya kirafiki.

    “Nchi hizi mbili si tu marafiki wa kuaminiana na kusaidiana lakini pia ni washirika wa maendeleo ya pamoja na ustawi wa pamoja,” Rais Xi amesema, huku akibainisha kwamba anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili na yuko tayari kufanya kazi na Rais mteule Muizzu ili kuendeleza urafiki wa kijadi, kuimarisha ushirikiano wa kivitendo na kusukuma maendeleo mapya ya ushirikiano wa kiwenzi na wa kirafiki wa pande zote kati ya nchi hizo mbili kwenye mwelekeo wa siku zijazo.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha