Lugha Nyingine
Kongamano la Mawasiliano ya Ustaarabu kati ya China na Cyprus lafanyika Nicosia
Picha hii iliyopigwa Oktoba 6. 2023 ikionyesha shughuli ya Kongamano la Mawasiliano ya Ustaarabu kati ya China na Cyprus huko Nicosia, Cyprus. (Xinhua/Wen Xinnian)
NICOSIA – Wakati Maonyesho ya Vitabu ya Nicosia yanapofanyika, Mji Mkuu wa Cyprus, Nicosia umeandaa Kongamano la Mawasiliano ya Ustaarabu kati ya China na Cyprus siku ya Ijumaa.
Wakati maonyesho hayo ya vitabu yameipa heshima China, kongamano hilo limewaleta pamoja watu mashuhuri kutoka katika siasa, wasomi na fasihi chini ya kauli mbiu ya "Kuchunguza Kuishi pamoja kwa Mapatano Kati ya Ustaarabu na Kati ya Binadamu na Mazingira ya Asili."
Katika hotuba yake, Zhang Jianchun, Naibu Waziri wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, amesisitiza haja ya kustawisha mazungumzo, maelewano na ushirikiano wa uchapishaji kati ya pande hizo mbili.
Pia ameangazia umuhimu mkubwa wa ustaarabu wa ikolojia, ambapo fasihi hutumiwa kama njia ya kuwezesha kubadilishana uzoefu ili kufanya Dunia kuwa safi na yenye kupendeza zaidi.
Irene Piki, Naibu Waziri katika Ikulu ya Cyprus, amesisitiza urithi wa sifa ya uhimilivu na uvumbuzi wa Cyprus na China, na kusisitiza jukumu muhimu la mabadilishano kati ya watu katika kuimarisha ushirikiano.
Tasos Christofides, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Cyprus, amesema kuwa mipango kama vile kongamano hilo inakuza uelewano, kuheshimiana na ushirikiano wa kuvuka mipaka ya kitamaduni.
Kongamano la Mabadilishano ya Ustaarabu kati China na Cyprus linaonyesha uhusiano wa pande zote wa kihistoria na kiutamaduni kati ya nchi hizo mbili na pia hutumika kama jukwaa la mazungumzo ya kiutamaduni na ushirikiano wa kiikolojia wa kimataifa.
Pia siku hiyo ya Ijumaa, Vitabu vya Ustawishaji wa Taifa la China, ambavyo vinaeleza mwelekeo wa China ya kisasa, vilitolewa kwa Chuo Kikuu cha Ulaya cha Cyprus na naibu waziri wa China.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma