Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping akutana na ujumbe wa wabunge wa Bunge la Seneti la Marekani
Rais Xi Jinping wa China akikutana na ujumbe wa wabunge wa Bunge la Seneti la Marekani unaoongozwa na Kiongozi wa Wabunge walio Wengi katika bunge hilo la Seneta Chuck Schumer kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Oktoba 9, 2023. (Xinhua/Zhai Jianlan)
Beijing - Rais Xi Jinping wa China amekutana na ujumbe wa wabunge wa Bunge la Seneti la Marekani unaoongozwa na Kiongozi wa Wabunge walio Wengi katika bunge hilo Seneta Chuck Schumer kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing siku ya Jumatatu.
Rais Xi amesisitiza kuwa uhusiano wa China na Marekani ni uhusiano muhimu zaidi wa pande mbili duniani. Na kwamba jinsi China na Marekani zinavyoendana pamoja ndivyo itaamua mustakabali wa binadamu. Amesema, ushindani na mapambano haviendani na mwenendo wa nyakati na hayawezi kutatua matatizo ya nchi binafsi na kushughulikia changamoto zinazoikabili Dunia.
“China inashikilia kuwa maslahi ya pamoja ya nchi hizi mbili ni makubwa kuliko migongano, na mafanikio ya China na ya Marekani ni fursa, siyo changamoto kwa kila upande,” Rais Xi amesema.
Amesema "Mtego wa Thucydides "(kila upande unaogopa kushambuliwa na upande mwingine, mwishowe kuonesha hali ya taabani ya usalama) unaweza kuepukika, na Sayari ya Dunia ni kubwa kuweza kutosha kushughulikia maendeleo husika na ustawi wa pamoja wa China na Marekani.
Rais Xi amesema kuimarika kwa uchumi wa Dunia baada ya janga la UVIKO-19, kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi na kusuluhisha maeneo hatari kwa migogoro ya kikanda na kimataifa kunahitaji uratibu na ushirikiano wa China na Marekani.
Ameeleza kuwa ustaarabu wa China umekuwa ukiendelea bila kukatika kwa zaidi ya miaka 5,000. Umekuwa kwa muda wote ukishikilia wazo la amani kuhusu kuendana na nyakati, kufundishana na kuwa na moyo wa ujumuishi, na kufanya mawasiliano na ushirikiano.
Rais Xi amesema, China itashikilia kufuata njia ya ujamaa wenye umaalum wa China, na kuendeleza maendeleo yake ya kisasa katika sekta zote, China imepata miujiza miwili ya maendeleo ya haraka ya kiuchumi na utulivu wa muda mrefu wa kijamii, mafanikio hayo yamewezekana kwa sababu nchi hiyo imepata njia ya maendeleo inayoendana na hali yake ya kitaifa.
Seneta Schumer na wajumbe wengine wa ujumbe huo wameeleza kufurahishwa kwao kutembelea nchi nzuri ya China na kuushukuru upande wa China kwa ukarimu wake, wakisema kuwa katika ziara yao wamehisi nguvu na uwezo wa kifursa wa maendeleo ya China.
Wametoa maoni na mapendekezo yao kuhusu masuala muhimu ya uhusiano kati ya China na Marekani, na walisema uhusiano huo una umuhimu mkubwa si tu kwa nchi hizo mbili, bali pia amani na maendeleo ya Dunia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma