<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Mashindano ya Hotuba yafanyika Kenya ?kwa ?kuonyesha mafanikio ya ?Kenya na China kujenga pamoja " Ukanda Mmoja,Njia Moja"

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 16, 2023

    Mashindano ya Hotuba yaliyoitwa " Ukanda Mmoja,Njia Moja: Hadithi Yangu ya China" yalifanyika huko Nairobi, Kenya, mnamo tarehe 13.

    Baada ya duru ya awali na nusu fainali, hatimaye washindani 10 wa Kenya walifanikiwa kufikia fainali, ambapo walisimulia hadithi zinazogusa moyo wa watu kuhusu kutimiza matumaini yao binafsi katika kazi zao za makampuni ya China na kushiriki katika ujenzi wa " Ukanda Mmoja,Njia Moja ".

    Concilia Owire atoa hotuba katika mashindano.(Xinhua)

    Concilia Owire atoa hotuba katika mashindano.(Xinhua)?

    Concilia Owire kutoka Kampuni ya Barabara na Madaraja ya China alinyakua taji la mashindano hayo . Akiwa mmoja wa madereva wa kike wa kwanza wa reli nchini Kenya, Owire alishuhudia mchakato wa ujenzi wa reli. Alisema, "Nilipoendesha treni na kufika kwenye kituo cha mwisho Nairobi, nilisisimka sana nikalia kwa furaha. Nilijua nimefikia lengo langu na ninaona majivuno , nchi yangu na mwalimu wangu wanajivunia kwa mafanikio yangu. Nitakumbuka daima wakati huo."

    Mwenyekiti wa Kikundi cha Urafiki wa Kenya na China katika Bunge la Kitaifa la Kenya, Shabir, alisema kwamba mashindano hayo yameonesha mafanikio mengi yaliyopatikana katika ushirikiano wa pamoja kati ya Kenya na China kwenye ujenzi wa Ukanda Mmoa, Njia Moja. China imesaidia ujenzi wa miradi mingi ya miundombinu nchini Kenya, miradi ambayo imechangia maendeleo ya kiuchumi ya Kenya .

    Mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kenya na China, na pia ni miaka 10 tangu pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” lilipotolewa.

    Concilia Owire akiwa kwenye mahojiano na waandishi wa habari baada ya mashindano.

    Concilia Owire akiwa kwenye mahojiano na waandishi wa habari baada ya mashindano.

    Tarehe 10 Oktoba, hafla ya kutoa tuzo kwa washindi wa Mashindano ya Hotuba "Hadithi Yangu ya China" ilifanyika Nairobi, Kenya.

    Tarehe 10 Oktoba, hafla ya kutoa tuzo kwa washindi wa Mashindano ya Hotuba "Hadithi Yangu ya China" ilifanyika Nairobi, Kenya.

    (Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

    Picha