<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais wa China akutana na Waziri Mkuu wa Msumbiji

    (CRI Online) Oktoba 20, 2023

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na Waziri Mkuu wa Msumbiji Bw. Adriano Maleiane ambaye alikuwa ziarani nchini China kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Baraza la 3 la Ushirikiano wa Kimataifa wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

    Rais Xi amepongeza ushirikiano kati ya China na Msumbiji na maendeleo yaliyopatikana katika ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

    Amesema China iko tayari kushirikiana na nchi za Afrika ikiwemo Msumbiji kujenga “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kuhimiza uungaji mkono wa utekelezaji wa hatua tatu za ushirikiano, ikiwemo mpango wa maendeleo ya viwanda wa Afrika, mpango wa China kufanya kazi na nchi za Afrika katika kufikia kilimo cha kisasa, na mpango wa ushirikiano wa kuandaa watu wenye ujuzi kati ya China na Afrika.

    Kwa upande wake Bw. Maleiane amesema, anafurahia kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Baraza la 3 la Ushirikiano wa Kimataifa wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na ziara yake imeimarisha ufahamu wake kuhusu China na pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na kuzidi kufahamu mtazamo wa mbali na wa kimkakati ya Rais Xi.

    Amesema, mapendekezo muhimu likiwemo pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na Pendekezo la Maendeleo ya Dunia yanasaidia nchi nyingi kuondokana na umaskini, kupata maendeleo ya kiuchumi na kuboresha maisha ya watu.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha