<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping?asisitiza wafanyakazi kushiriki katika ustawishaji mkubwa wa Taifa

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 24, 2023

    Rais Xi Jinping wa China akizungumza na uongozi mpya wa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China na kutoa hotuba muhimu mjini Beijing, China, Oktoba 23, 2023. (Xinhua/Ju Peng)

    Rais Xi Jinping wa China akizungumza na uongozi mpya wa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China na kutoa hotuba muhimu mjini Beijing, China, Oktoba 23, 2023. (Xinhua/Ju Peng)

    Rais Xi Jinping wa China, amesisitiza kuzingatia uongozi wa jumla wa Chama cha kikomunisti cha China kwa mashirikisho ya wafanyakazi na kuhamasisha mamia ya mamilioni ya wafanyakazi wa China kushiriki kwa nguvu katika kazi kubwa ya ujenzi wa nchi yenye nguvu na ustawi wa Taifa.

    Rais Xi ameyasema hayo jana alipozungumza na uongozi mpya wa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China (ACFTU).

    “Maendeleo ya harakati za wafanyakazi wa China yalikuwa chini ya uongozi wa Chama, na mashirikisho ya wafanyakazi ni mashirika ya umma ya wafanyakazi yanayoongozwa na Chama” amesema.

    Rais Xi amesisitiza umuhimu wa kutilia maanani uongozi mzima wa Chama kwa mashirikisho ya wafanyakazi, na kutoyumbishwa au kukengeuka kutoka katika muktadha huo wakati wowote au kwa hali yoyote.

    Amesema kwa kuzingatia sera ya msingi ya kutegemea wafanyakazi kwa moyo wote, ni lazima juhudi zifanywe ili kuwahimiza wafanyakazi kushiriki kikamilifu katika kazi kubwa ya kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu na ustawishaji wa Taifa katika sekta zote.

    Amebainisha kuwa tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC ulipofanyika, wafanyakazi wamekuwa nguvu kuu katika maendeleo ya lengo kuu la Chama na nchi chini ya uongozi thabiti wa Kamati Kuu ya CPC. Amesema harakati za wafanyakazi wa China zimepata mafanikio ya kihistoria, na kazi ya mashirikisho ya wafanyakazi imepata maendeleo makubwa.

    Rais Xi amesisitiza kuwa wafanyakazi ndiyo watengenezaji wakuu wa utajiri wa kijamii, na maendeleo yanayoonekana zaidi katika kuleta ustawi wa pamoja kwa watu wote, lazima kwanza yaonekane katika mamia ya mamilioni ya watu wanaofanya kazi.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha