Lugha Nyingine
Mwanadiplomasia wa Afrika na wageni wahudhuria shughuli za kitamaduni Mjini Xi'an, Kaskazini Magharibi mwa China
Wanadiplomasia wa Afrika na China na wageni wengine waalikwa wakihudhuria mazungumzo huko Xi'an, Mji Mkuu wa Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China, Novemba 4, 2023. (Xinhua)
XI'AN - Wanadiplomasia wa China na Afrika na wageni wengine waalikwa walihudhuria mazungumzo huko Xi'an, Mji Mkuu wa Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China siku ya Jumamosi, wakipata uzoefu wa shughuli ya jadi ya utengenezaji wa chai na kutazama maonyesho ya urithi wa utamaduni usioshikika.
Balozi wa Zambia nchini China, Iven Zyuulu, wawakilishi wa Afrika wa washindi wa shindano la video fupi kuhusu urafiki kati ya China na Afrika, na Balozi wa zamani wa China katika Jamhuri ya Kongo Ma Fulin walihudhuria shughuli hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Maonyesho ya Jukwaani wa Yisu, ambalo ni klabu ya opera ya Qinqiang iliyoanzishwa Mwaka 1912.
Opera ya Qinqiang na maonyesho ya kivuli cha vikaragosi yalikuwa miongoni mwa maonyesho ya urithi wa utamaduni usioshikika waliyotazama.
Wageni hao kutoka ndani na nje ya China pia walibadilishana maoni yao kuhusu urafiki kati ya China na Afrika na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI).
Zambia ni nchi ya kwanza Kusini mwa Afrika kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Jamhuri ya Watu wa China na ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili umeendelezwa mbele, kama alivyosema Balozi Zyuulu.
Amesema kuwa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) inawakilisha kumbukumbu ya urafiki kati ya nchi hizo mbili, na Zambia iko tayari kushirikiana na China kuendeleza ushirikiano wa BRI.
Kwa upande wake Balozi Ma amesema kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika katika nyanja mbalimbali utaimarishwa zaidi chini ya mfumo wa BRI ili kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma