<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Xi Jinping asisitiza ujenzi wa mfumo wa utaratibu wa kisheria wa China unaohusiana na mambo ya nje

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 29, 2023

    Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesisitiza haja ya kuimarisha ujenzi wa mfumo wa utaratibu wa kisheria wa China unaohusiana na mambo ya nje, alipokuwa akiongoza semina elekezi ya 10 ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC siku ya Jumatatu.

    Xi amesisitiza kuweka mazingira ya utawala unaofuata sheria na mazingira mazuri ya nje kwa ajili ya kusukuma mbele maendeleo ya mambo ya kisasa ya China, amesisitiza kwamba kuimarisha utaratibu wa kisheria unaohusiana na mambo ya nje ni mahitaji ya muda mrefu kwa ajili ya kujenga Taifa la China lenye nguvu na kuendeleza ustawishaji wa taifa hilo kupitia Njia ya Maendeleo ya mambo ya Kisasa ya China.

    Amesisitiza zaidi umuhimu wa kuendeleza kwa haraka ujenzi wa mfumo wa utaratibu wa kisheria unaohusiana na mambo ya nje katika kuharakisha kufungua mlango kwa kiwango cha juu na kushughulikia hatari na changamoto za nje.

    Akitoa wito wa kutilia maanani umuhimu na udharura wa suala hilo, Xi amesisitiza ujenzi wa mfumo wa utaratibu wa kisheria unaohusiana na mambo ya nje na uwezo unaokidhi mahitaji ya maendeleo yenye ubora wa juu na ufunguaji mlango wa kiwango cha juu wa China.

    Profesa kutoka Chuo Kikuu cha Wuhan alitoa mhadhara, ambapo wajumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC walikuwa na majadiliano.

    Akizungumza baada ya majadiliano hayo, Xi ameeleza kuwa mfumo wa utaratibu wa kisheria unaohusiana na mambo ya nje ni sehemu muhimu ya mfumo wa sheria wa China na kusisitiza kuwa lengo la msingi la kuendeleza usimamizi wa kisheria katika mambo yanayohusiana na nje ni kulinda maslahi ya nchi na wananchi kupitia njia za kisheria, kuwezesha maendeleo katika usimamizi wa kimataifa kwa mujibu wa sheria, na kuendeleza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Amesisitiza kujenga mfumo wa utaratibu wa kisheria wenye uwazi unaohusiana na mambo ya nje, kuimarisha ulinzi wa haki miliki ya ubunifu, kulinda haki na maslahi halali ya kampuni za kigeni zinazowekeza nchini China, na kuharakakisha kuweka mazingira ya biashara yenye mwelekeo wa soko, msingi wa kisheria na yaliyo ya kimataifa.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha