<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais wa China atuma ujumbe wa pongezi kwa mkutano wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina

    (CRI Online) Novemba 30, 2023

    Rais Xi Jinping wa China ametoa ujumbe wa pongezi kwa mkutano wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na watu wa Palestina uliofanyika Jumatano kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

    Rais Xi amesema suala la Palestina ni kiini cha suala la Mashariki ya Kati, na linahusiana na haki na usawa wa kimataifa na, kwamba tatizo sugu la mgogoro kati ya Palestina na Israel linatokana watu wa Palestina kunyimwa kutimiza haki halali za kitaifa za kuunda taifa lao huru.

    Katika ujumbe huo Rais Xi amesema, mzunguko wa mapigano kati ya Palestina na Israel umethibitisha kuwa njia pekee ya kutimiza usalama wa kudumu ni kushikilia msimamo wa usalama wa pamoja.

    Amesema, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua za dharura na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatakiwa kubeba wajibu, ili kufanya juhudi zote kufikia usimamishaji wa vita, kulinda usalama wa raia wa kawaida, kuzuia maafa ya kibinadamu.

    Amesema, juu ya msingi huo, mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel yanapaswa kuanza tena haraka iwezekanavyo na haki ya Wapalestina ya kuunda taifa lao na kuishi na haki yao ya kurejea katika ardhi yao inabidi irejeshwe haraka iwezekanavyo.

    Rais Xi amesisitiza kuwa China kama ambavyo imekuwa ikifanya ziku zote, inaunga mkono kithabiti harakati za watu wa Palestina kurejesha haki halali za kitaifa na kwamba suluhu pekee ya kimsingi ya suala la Palestina iko katika kuunda taifa huru la Palestina lenye mamlaka kamili kwenye msingi wa mipaka iliyowekwa mwaka 1967 na Jerusalem Mashariki ikiwa ni mji wake mkuu.

    Pia amesema mahitaji ya kiuchumi ya Palestina na shughuli za kimaisha za watu zinapaswa kuhakikishwa, na jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuongeza msaada wa maendeleo na wa kibinadamu kwa Palestina.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha