<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais wa China ampongeza Andry Nirina Rajoelina kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Madagascar

    (CRI Online) Desemba 07, 2023

    Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa Andry Nirina Rajoelina kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Madagascar.

    Kwenye salamu hizo, Rais Xi amesema, katika miaka ya karibuni, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa ukiendelea kwa kasi, mabadilishano na ushirikiano katika nyanja mbalimbali umepata matunda mazuri na pande hizo mbili zimeungana mkono kithabiti katika maslahi muhimu na mambo makubwa yanayofuatiliwa nazo.

    Pia Rais Xi amesema, anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Madagascar, na yuko tayari kushirikiana na Rais Rajoelina katika kuhimiza uhusiano wa ushirikiano wa pande zote kati ya nchi hizo kupata maendeleo makubwa zaidi, na kunufaisha zaidi watu wa nchi mbili.

    (Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

    Picha