<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping kufanya ziara ya kiserikali nchini Vietnam Desemba 12-13

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 08, 2023

    BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Hua Chunying ametangaza siku ya Alhamisi kwamba, Rais Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), atafanya ziara ya kiserikali nchini Vietnam kuanzia Desemba 12 hadi 13 kutokana na mwaliko wa Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam Nguyen Phu Trong na Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Kijamaa ya Vietnam Vo Van Thuong.

    Wang Wenbin, msemaji mwingine wa wizara hiyo, amesema katika mkutano na waandishi wa habari wa siku ya Ijumaa kwamba baada ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha CPC mwaka jana, Rais Xi alimwalika Trong kufanya ziara nchini China na viongozi hao wawili kwa pamoja waliweka dira ya ushirikiano wa kimkakati wa China na Vietnam.

    Wang amesema kuwa mwaka huu kumekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara ya ngazi ya juu, mawasiliano ya karibu kati ya idara na mikoa mbalimbali, na ushirikiano wa kina katika nyanja mbalimbali, ambao umeleta manufaa halisi kwa watu wa pande mbili.

    Dunia iko katika kipindi kipya cha misukosuko na mageuzi, huku kukiwa na kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na utulivu na uhakika, Wang amesema, huku akiongeza kuwa China na Vietnam zote ni nchi za kijamaa na zote zinaendeleza mageuzi, na kutumia dhana mpya na njia mpya kwa kubadilisha hali ilivyo ya sasa na kuhimiza maendeleo na uvumbuzi kupata matokeo mazuri zaidi. Kuimarisha mshikamano na urafiki, kuendeleza kwa kina ushirikiano wa kunufaishana kunaendana na maslahi ya pamoja ya pande zote mbili, na kunasaidia kulinda amani, utulivu na ustawi wa kanda na Dunia nzima.

    Msemaji Wang amesema, katika ziara hiyo, Rais Xi atafanya mazungumzo na Katibu Mkuu Nguyen Phu Trong na Rais wa Serikali Vo Van Thuong, na kukutana na Waziri Mkuu wa Vietnam, Pham Minh Chinh na Spika wa Bunge la Taifa Vuong Dinh Hue, ambapo pande hizo zitajadili kupandisha hadhi ya uhusiano kati ya China na Vietnam, na kuhimiza ushirikiano wa kimkakati katika maeneo ya siasa, usalama na masuala ya bahari na mengineyo.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha