<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping ahimiza vyombo vya mahakama, mwendesha mashtaka na usalama wa umma kulinda ustawishaji wa Taifa la China

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 15, 2024

    BEIJING - Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amevitaka vyombo vya mahakama, mwendesha mashtaka na usalama wa umma kushikilia uongozi kamili wa Chama na kuupa ustawi wa Taifa la China dhamana thabiti ya usalama, huku akitoa wito kwa maofisa katika vyombo hivyo kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu na kuonyesha juhudi nzuri.

    Rais Xi ametoa maagizo hayo muhimu kwenye mkutano kuhusu kazi za mahakama, mwendesha mashtaka na usalama wa umma, ambapo pia amehimiza juhudi za kulinda kithabiti usalama wa nchi, kuongeza werevu na uelewa wa kisiasa, kuzuia na kushughulikia hatari kubwa za kiusalama. Pia ametoa wito wa kudumisha utulivu wa kijamii na kulinda haki na maslahi halali ya watu.

    Usawa na haki kwenye jamii vinapaswa kulindwa na kuhimizwa, na ni lazima kulinda umoja wa utekelezaji wa sheria wa nchi, amesema Xi, pia ameongeza kuwa utaratibu wa uchumi wa soko huria wa kijamaa unapaswa kulindwa kwa mujibu wa sheria, na ujenzi wa mazingira ya biashara yanayofuata sheria unapaswa kuboreshwa.

    Rais Xi pia ametoa wito wa kuimarishwa kwa ujenzi wa kisiasa wa Chama katika vyombo vya mahakama, mwendesha mashtaka na usalama wa umma.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha