<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi Jinping asisitiza kuhimiza maendeleo yenye sifa bora ya mambo ya fedha ya China

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 17, 2024

    Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akihutubia ufunguzi wa semina  ya mada maalum kuhusu  kuhimiza maendeleo yenye  sifa bora ya mambo ya fedha ya China,  semina hiyo ya maofisa viongozi wa  ngazi ya mikoa na wizara  inafanyika katika Chuo cha Chama ya Kamati Kuu ya CPC mjini Beijing, China, Januari 16, 2024. (Xinhua/Ju Peng)

    Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akihutubia ufunguzi wa semina ya mada maalum kuhusu kuhimiza maendeleo yenye sifa bora ya mambo ya fedha ya China, semina hiyo ya maofisa viongozi wa ngazi ya mikoa na wizara ilifanyika katika Chuo cha Chama ya Kamati Kuu ya CPC mjini Beijing, China, Januari 16, 2024. (Xinhua/Ju Peng)

    BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), Jumanne wakati akihutubia ufunguzi wa semina ya mada maalum inayofanyika katika Chuo cha Chama cha Kamati Kuu ya CPC, amesisitiza kuendelea kujitoa kwa ajili ya njia ya maendeleo ya mambo ya fedha yenye umaalum wa China na kuhimiza maendeleo yenye sifa bora ya mambo ya fedha ya China.

    Rais Xi amesisitiza kwenye semina hiyo ya maofisa viongozi wa mikoa na wizara kuwa, njia ya maendeleo ya mambo ya fedha yenye umaalum wa China si kama tu inafuata kanuni za hali ilivyo za maendeleo ya mambo ya fedha ya zama tulizonazo, bali pia ina sifa wazi ya kufaa kwa hali ya nchi ya China, na kimsingi ni tofauti na muundo wa mambo ya fedha wa nchi za Magharibi, tunatakiwa kujiamini kithabiti, kuendelea na utafiti katika uzoefu ili kukamilisha muundo wetu na kupanua zaidi njia hii.

    Rais Xi amedhihirisha kuwa, tangu kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC, juhudi zimefanywa ili kuzidisha uelewa wa kila mara juu ya msingi wa mambo ya fedha ya kijamaa yenye umaalum wa China, na kuhimiza uzoefu na uvumbuzi wa mambo ya fedha katika masuala ya matumizi halisi, nadharia na utaratibu, China imekusanya uzoefu wa thamani, na hatua kwa hatua kuunda njia ya maendeleo ya mambo ya fedha yenye umaalum wa China. Ameeleza kuwa nchi yenye nguvu kubwa ya mambo ya fedha inapaswa kutegemea msingi imara wa kiuchumi, kuwa na nguvu kubwa ya kuongoza duniani katika uchumi, sayansi na teknolojia na nguvu ya ujumla ya nchi.

    Amesisitiza kufanya juhudi za kuzuia na kupunguza hatari za mambo ya fedha, haswa hatari za kimfumo.

    Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akihutubia hafla ya ufunguzi wa semina ya mada maalum kuhusu  kuhimiza maendeleo yenye  sifa bora ya mambo ya fedha ya China,  semina hiyo ya maofisa viongozi wa ngazi ya mikoa na wizara, inafanyika katika  Chuo cha Chama ya Kamati Kuu ya CPC  mjini Beijing, China, Januari 16, 2024. (Xinhua/Shen Hong)

    Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akihutubia hafla ya ufunguzi wa semina ya mada maalum kuhusu kuhimiza maendeleo yenye sifa bora ya mambo ya fedha ya China, semina hiyo ya maofisa viongozi wa ngazi ya mikoa na wizara, inafanyika katika Chuo cha Chama ya Kamati Kuu ya CPC mjini Beijing, China, Januari 16, 2024. (Xinhua/Shen Hong)

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha