<abbr id="aakgw"><source id="aakgw"></source></abbr>
<dl id="aakgw"><tr id="aakgw"></tr></dl>
<li id="aakgw"></li>
  • <li id="aakgw"></li>
    <bdo id="aakgw"></bdo>
    <sup id="aakgw"><bdo id="aakgw"></bdo></sup><code id="aakgw"></code>

    Rais Xi aagiza utafutaji na uokoaji wa pande zote wa watu wasiojulikana waliko katika maporomoko ya ardhi Kusini Magharibi mwa China

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 23, 2024

    BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) ameagiza kutafuta na kuokoa kwa nguvu zote watu wote wasiojulikana waliko kwenye maporomoko ya ardhi katika Wilaya ya Zhenxiong, Mkoa wa Yunnan, Kusini Magharibi mwa China yaliyotokea mapema siku ya Jumatatu.

    Watu jumla ya 47 hawajulikani walipo baada ya maporomoko hayo kuzika nyumba za familia 18.

    Rais Xi ameagiza kufanyika juhudi za haraka za uokoaji ili kupunguza madhara. Pia ametaka kuimarishwa kwa ufuatiliaji na tahadhari ya mapema pamoja na mbinu za kisayansi katika juhudi za utafutaji na uokoaji ili kujikinga na majanga ya pili.

    Katika maagizo yake, Rais Xi ametoa wito wa kuhakikisha hatua zinazofaa za kuzifariji familia za waathirika na kuwapa makazi mapya wale walioathirika huku akisema kuwa majanga ya asili, ajali za barabarani na matukio ya usalama kazini yanaweza kutokea wakati ambapo likizo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China inapokaribia na kutokana na athari mbaya ya mawimbi ya baridi kali.

    Ameitaka mikoa na idara husika kufuatilia kwa makini hatari zinazoweza kutokea na kubeba wajibu wao ili kuzuia maafa makubwa na kuhakikisha usalama wa maisha na mali za watu.

    Naye Waziri Mkuu wa China Li Qiang pia ametoa wito wa kufanya juhudi za uokoaji na utoaji msaada. Li, ambaye pia ni Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, amewataka waokoaji wafanye juhudi kwa wawezavyo bila kupoteza muda hata kidogo katika kutafuta watu wasiojulikana walipo na kujaribu kila wawezalo kupunguza madhara.

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

    Picha